logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Matokeo ya siku ya nne ya kombe la EURO 2020

Mataifa sita yalihusishwa kwenye siku ya Jumatatu kwenye michuano ya EURO 2020

image
na Radio Jambo

Habari14 June 2021 - 20:29

Muhtasari


•Mechi kati ya Poland na Slovakia iliandikisha kadi nyekundu ya kwanza tangu michuano ya EURO 2020 kuanza Ijumaa wiki iliyopita

•Mechi mbili kubwa zitapigwa siku ya Jumanne. Hungaria itaalika Ureno huku mabingwa wa kombe la dunia mwaka wa 2018, Ufaransa, wakialika mabingwa wa kombe la dunia mwaka wa  2014, Ujeumani mwendo wa saa nne usiku.

Robert Lewandoski wa Poland baada ya kupoteza mechi dhidi ya Slovakia

Mataifa sita yalihusishwa kwenye siku ya nne ya kombe la EURO 2020.

Uskoti, Ucheki, Poland, Slovakia, Uhispania na Uswidi izilishiriki kwenye michuano yao ya kwanza siku ya Jumatatu.

Mechi ya kwanza ilikuwa kati ya Uskoti na Ucheki ambapo wenyeji Uskoti walipokea kichapo cha mabao mawili kwa sufuri. Mabao mawili ya Uskoti yalifungwa na mshambulizi wa Bayern Leverkusen Patrik Schick.

Poland ilikaribisha Slovakia kwenye mchuano wa pili wa siku ambao ulichezwa saa moja usiki masaa ya Afrika Kusini.Slovakia iliweza kuwapiga wenyeji mabao mawili kwa moja huku bao la kujifunga la Wojciech Szczesny na lile la mlinzi wa Inter Milan,  Milan Skriniar yakifanikisha ushindi huo.

Karol Linetty alifungia Poland bao moja la kufutia machozi.

Mechi kati ya Poland na Slovakia iliandikisha kadi nyekundu ya kwanza tangu michuano ya EURO 2020 kuanza Ijumaa wiki iliyopita. Grzegorz Krychowiak alipatiwa kandi ya majano kwa mara ya pili katika dakika ya 62 na kuondolewa uwanjani na refa Ovidiu Hategan.

Mchuano wa mwisho wa siku ya Jumatatu ulikuwa kati mabingwa mara tatu wa kombe la Euro, Uhispania na Uswidi.Licha ya majaribio mengi ya kufunga haswa kutoka upande wa Uhispania, mechi ile iliandikisha sare tasa.

Timu hizo mbili ni baadhi ya timu ambazo zinaangaziwa sana kutokana na umaarufu wa wachezaji wake.

Mechi mbili kubwa zitapigwa siku ya Jumanne. Hungaria itaalika Ureno huku mabingwa wa kombe la dunia mwaka wa 2018, Ufaransa, wakialika mabingwa wa kombe la dunia mwaka wa  2014, Ujeumani mwendo wa saa nne usiku.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved