Orodha ya wanakandanda waliozirai wakiwa uwanjani

Muhtasari
  • Orodha ya wanakandanda waliozirai wakiwa uwanjani
Image: Hisani

Wachezaji wengi wa soka mara moja wamezirai uwanjani, mara ya hivi karibuni Jumamosi usiku wakati wa Euro 2020 katika mechi kati ya Denmark na Finland.

Katika makala haya tutazingatia wachezaji ambao wamewahi zirai uwanjani.

1.Christian Eriksen

Eriksen alizirai uwanjani wakati akiwakilisha nchi yake Denmark katika mechi ya euro 2020 dhidi ya Finland.

Tukio hilo lilifanyika  usiku wa Juni 12, kuanguka kwake kwa ghafla kulikuwa na mshtuko wa kweli kwa ulimwengu wanakandanda.

2.Miklos Feher

Feher alizirai akichezea klabu  ya Kireno Benfica mwaka 2004. Mchezaji huyo wa Hungary alikimbizwa hospitali lakini aliaga dunia akipokea matibabu.

3.Antonio Puerta

Mchezaji wa zamani wa Sevilla mara moja alizirai uwanjani wakati akicheza dhidi ya Getafe katika Laliga

4.Bafetimbi Gomis 

Bafetimbi amezirai uwanjani i mara kadhaa. Mshambuliaji wa Kifaransa alizirai wakati wa mchuano kati ya Swansea, Al-Hilal na Galatasaray