logo

NOW ON AIR

Listen in Live

FKF yasimamisha kazi maafisa 5 wa FKF-PL waliokabiliwa na tuhuma za udanganyifu kwenye mechi

FKF kwa ushirikiano na FIFA wameanza uchunguzi kubaini iwapo ni kweli watano hao walihusika kwenye udanganyifu wa mechi zilizotajwa

image
na Samuel Maina

Michezo31 July 2021 - 08:07

Muhtasari


  • •Watano hao ikiwemo refa wa FIFA Raymond Onyango wamesimamishwa kazi ili kupatia nafasi uchunguzi kuendelea kufuatia tuhuma za udanganyifu kwenye mechi za kandanda nchini.
  • •Wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na Samuel Mwaura, Isaac Memusi, Collins  Opiyo na Japeth Juma.

Shirikisho la soka nchini, FKF, limesimamisha kazi maafisa watano wanaosimamia michuano ya ligi ya soka nchini, FKF-PL.

Watano hao ikiwemo refa wa FIFA Raymond Onyango wamesimamishwa kazi ili kupatia nafasi uchunguzi kuendelea kufuatia tuhuma za udanganyifu kwenye mechi za kandanda nchini.

Wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na Samuel Mwaura, Isaac Memusi, Collins  Opiyo na Japeth Juma.

FKF kwa ushirikiano na FIFA wameanza uchunguzi kubaini iwapo ni kweli watano hao walihusika kwenye udanganyifu wa mechi zilizotajwa.

FKF imesema kuwa imesimamisha kazi watano hao kama tahadhari.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved