Kiungo mshambuliaji wa Ureno mwenye mbio za duma, Christiano Ronaldo amezungumzia kuhusu uwezekano wa taifa lako kushindwa ubingwa wa kombe la dunia na pia kutathmini kile kitakachotokea katika maisha yake.
Akizungumza na mwanahabari Piers Morgan ambaye alimuuliza atajihisi vipi endapo timu ya taifa la Ureno itafika kwenye fainali za kipute cha kombe la dunia nchini Qatar na kuibuka washindi, Ronaldo alisema kwamba endapo hilo litatokea basi atakuwa ni binadamu mwenye furaah zaidi duniani.
Morgan alitaka kujua kile kitakachokuwa kikizungumza kwenye akili zake ikitokea taifa la Ureno ambaloRonaldo ndiye kapteni watakutana kwenye fainali na Argentina ambayo nahodha wao ni Lionel Messi – mtani wa jadi wa Ronaldo katika malimwengu ya soka.
“Vizuri zaidi, itakuwa ndoto nzuri sana. Hata kama mchezaji yeyote atafunga bao la ushindi sijali, bora tu iwe ni Ureno inabeba ubingwa wa dunia. Hata kama ni kipa wetu atafunga bao la ushindi mimi nitakuwa mtu mwenye furaha zaidi duniani. Lakini kama hili litatokea…nitamaliza safari yangu ya kucheza kandanda siku hiyo hiyo. Nitastaafu! Ukweli asilimia mia,” Christiano Ronaldo alisema.
Pia alitumia nafasi hiyo kumsifia mwenzake wa Argentina Lionel Messi na kusema kwamba ni mchezaji wa kiwango cha juu zaidi. Alisema kwamba uhusiano wao hauwezi ukalinganishwa na kitu chochote kwa sababu wamekuwa wakishindana kwa miaka 16 iliyopita.
Ronaldo alisema anaheshimu sana jinsi Messi anamzungumzia kwa mazuri na hata kufichua kuwa hata wake zao wote wanatoka Argentina na wanaheshimiana pakubwa.