Rubiales asimamishwa kazi na Fifa

Alisema kwamba "hakuna wakati ambapo nilitaka kumuinua (kumwinua) rais".

Muhtasari
  • Inaongeza kuwa haitasema lolote kuhusu hatua zozote za kinidhamu hadi kesi dhidi ya Rubiales itakapokamilika. 

Katika dakika chache zilizopita tumesikia kwamba Luis Rubiales amesimamishwa kushirki katika "shughuli zote zinazohusiana na soka katika ngazi ya kitaifa na kimataifa" kwa kipindi cha siku 90 na Kamati ya nidhamu ya Fifa.

Fifa inasema imewasilisha uamuzi wake kwa Luis Rubiales, shirikisho la soka la Uhispania na shirikisho la soka barani Ulaya (Uefa).

Inaongeza kuwa haitasema lolote kuhusu hatua zozote za kinidhamu hadi kesi dhidi ya Rubiales itakapokamilika.

Fifa tayari ilikuwa imefungua kesi za kinidhamu dhidi ya Rubiales kwa kitendo chake wakati wa utoaji wa medali ya Kombe la Dunia la Wanawake mnamo Agosti 24, alipombusu kiungo wa kati Jenni Hermoso kwenye midomo.

Anasema hakukubali busu hilo - Rubiales anasema lilikubalika.

Luis Rubiales amejitetea kwa kudai kuwa Jenni Hermoso alimuinua kutoka chini wakati wa kukabidhiwa kombe (kumbatio lao lipo kaka picha hii ).

"Jenni ndiye aliyeniinua," alisema wakati wa mkutano wa shirikisho la soka la Uhispania jana.

"Nilimwambia 'asahau penalti (ambayo alikosa katika fainali ya Kombe la Dunia)' na nikamwambia 'busu kidogo?' na akasema 'Sawa'."

Kisha akambusu kwenye midomo yake.

Hermoso alikanusha mazungumzo yote katika taarifa ya Ijumaa, akisema kwamba maneno ya Rubiales "yalikuwa ya uwongo kabisa na ni sehemu ya utamaduni wa hila ambao yeye mwenyewe ameunda".

Alisema kwamba "hakuna wakati ambapo nilitaka kumuinua (kumwinua) rais".

Asubuhi ya leo, shirikisho la soka la Uhispania liliita kauli ya Hermoso "uongo", na ikasema itachukua hatua za kisheria kuhusu maoni yake. Ilirudia dai kwamba alitumia nguvu kuinua miguu ya Rubiales kutoka ardhini.