Robert Lewandowski alifunga mabao matatu katika kipindi cha pili kuipa nguvu Barcelona katika ushindi wa kusisimua wa 4-2 dhidi ya Valencia Jumatatu usiku. Ushindi wa mabingwa hao unazuia viongozi Real Madrid nafasi ya kuchukua taji kwa kushinda tu dhidi ya Cadiz Jumamosi ijayo. Los Blancos wanaongoza jedwali kwa pointi 11 mbele ya Barcelona.
Fermin Lopez aliifungia wenyeji bao la kwanza kabla ya mshambuliaji wa Valencia Hugo Duro kusawazisha na Pepelu kufunga kutoka kwa penalti kubadilisha mwelekeo wa mchezo.
Kipa wa Valencia, Giorgi Mamadashvili alitolewa nje kwa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha kwanza. Lewandowski alisawazisha wenyeji muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza.
"Nadhani timu ilifanya vizuri. tulikosa utulivu, amani, lakini nimeridhika na hali ya timu," kocha wa Barcelona Xavi aliiambia DAZN.
Wageni Valencia, wa nane na wakilenga kufuzu kwa soka la Ulaya msimu ujao, walipata nafasi bora mapema lakini walishdwa kuzitumia vizuri.
Barcelona walichukua uongozi wakati Lopez alipofunga kichwa kutoka krosi ya Raphinha.
Valencia haraka walisawazisha baada ya kosa kubwa la kipa wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, ambaye alikimbia nje ya sanduku lake kujaribu kuzuia pasi ndefu.
Aliwasili kwanza lakini alishindwa jaribio lake la kumvisha kanzu Duro na mshambuliaji akadhibiti mpira na kumshinda Ronald Araujo kabla ya kufunga.
"Kipindi cha kwanza, hatukuwa na nafasi nyingi kwenye safu ya ushambuliaji, lakini muhimu zaidi ni ikiwa utapoteza bao moja au mawili, tunaweza kufunga matatu au manne kila wakati," Lewandowski aliiambia DAZN.
"Ikiwa tutafunga mabao mengi, ni rahisi zaidi kwa kila mtu."
Ushindi wa Barcelona uliwapeleka pointi mbili mbele ya majirani zao Girona, wa tatu, ambao watawatembelea Jumamosi ijayo.
Wachezaji hao wanasaka kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa, ambayo wanaweza kupata ushindi huo, ambao pia unaweza kuipa Madrid ubingwa.
"Utakuwa mchezo mzuri sana, timu mbili zinatarajia kwenda kushambulia," alisema Xavi, ambaye timu yake ilipoteza 4-2 nyumbani dhidi ya Girona mnamo Desemba.
"Itakuwa tamasha kubwa, kama tulivyoona huko Montjuic."