logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vincent Kompany,McKenna,Thomas Frank miongoni mwa wakufunzi watarajiwa Chelsea

Klabu ya Chelsea inatarajiwa kumtaja mkufunzi wao hivi karibuni baada ya Pochettino kuondoka.

image
na Davis Ojiambo

Michezo22 May 2024 - 09:09

Muhtasari


  • •Chelsea kumtaja mkufunzi wao hivi karibuni
  • •Pochettino aliachishwa kazi baada ya madai ya kutoelewana na wakubwa wake.
Kocha Mauricio Pochettino

Chelsea ipo mawindoni kumtafuta mkufunzi mpya, baada ya Mauricio Pochettino kuondoka,usiku wa kuamkia Jumatano.

Kulingana na ripoti za mwanahabari maarufu,Fabrizio Romano,kulikuwepo na kutokuelewana baina ya mkufunzi Pochettino na wasimamizi wa klabu hio.Dira,mipango ya baadaye kati ya Pochettino na wasimamizi wake haikuambatana hivo kumuachisha kazi mara moja.

Inasemekana kuwa Pochettino alitaka ahusishwe kwenye mambo ya uhamisho wa wachezaji ila wakubwa wake hawakupendelea jambo hilo.

Wachezaji kadhaa wameonyesha kutofurahishwa na kufurushwa kwa kocha huyo akiwemo Nicholas Jackson.Ikizingatiwa kuwa hisia za mkufunzi huyo na wachezaji wake zilikuwa zimeimarika hivi majuzi.

Kwa sasa klabu inaamini kumtaja kocha anayeamini vipaji vya vijana wadogo,umilisi wa asilimia kubwa uwanjani utasaidia timu hiyo kufika viwango vya juu.

Hakuna mawasiliano rasmi yaliyofanyika baina ya Thomas Tuchel,Antonio Conte,Jose Mourinho na Hansi Flick ambao kwa sasa wapo huru licha ya uvumi kuenea.

Aidha,mkufunzi wa Brentford Thomas Frank,Kieran McKenna wa Ipswich town na Vincent Kompany wamehusishwa ila hakuna chapisho rasmi kwa sasa.

Wagombea zaidi watajadiliwa kati ya wamiliki na wakurugenzi wa klabu hio ili kufanya maamuzi ya mwisho.Je,ungependelea kocha yupi aje stamford Bridge?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved