logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Euro 2024: Wachezaji 11 wenye asili ya Afrika watakaochezea mataifa ya Ulaya

Watakashiriki Euro 2024, kuanzia Juni 14 hadi Julai 14 nchini Ujerumani.

image
na Samuel Maina

Michezo07 June 2024 - 04:37

Muhtasari


  • •Brice Samba, kipa wa RC Lens, aliitwa kwenye timu ya Ufaransa kwa mara ya kwanza na kocha Didier Deschamps Machi 2023.
  • •Denis Zakaria, 26, alizaliwa huko Geneva na mama kutoka Sudan Kusini na baba wa Congo.

Miongoni mwa wachezaji waliochaguliwa kucheza michuano ya soka ya Mataifa ya Ulaya (Euro 2024), baadhi yao wana asili ya Afrika na wangeweza kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika katika nchi zao za asili kama wangetaka.

BBC inakupa majina ya wachezaji 11 wenye asili ya Afrika watakaoshiriki Euro 2024, kuanzia Juni 14 hadi Julai 14 nchini Ujerumani.

Brice Samba (Ufaransa-Congo)

Maelezo ya picha,Brice Samba kipa nambari mbili wa Ufaransa akijifua kabla ya mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Ufaransa na Ujerumani Machi 23, 2024 huko Lyon.

Brice Samba, kipa wa RC Lens, aliitwa kwenye timu ya Ufaransa kwa mara ya kwanza na kocha Didier Deschamps Machi 2023.

Kipa namba mbili wa Ufaransa alizaliwa na wazazi kutoka Congo Aprili 25, 1994 huko Linzolo, kilomita 20 kusini mwa Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Congo.

Alifunzwa katika klabu ya Le Havre, Brice Samba alicheza Marseille, Caen na Nottingham Forest ya Ligi ya Uingereza, na sasa anachezea RC Lens ya Ufaransa tangu 2022.

Brice Samba 30 ambaye hakuwahi kuitwa kabla, atacheza katika mashindano ya kimataifa kwa mara ya kwanza kama kipa namba mbili nyuma ya Mike Maignan.

Antonio Rüdiger (Ujerumani - Sierra Leone)

Antonio Rüdiger moja ya mabeki bora duniani, alizaliwa Ujerumani mwaka 1993, na mama wa Sierra Leone ambaye alikimbia vita vya wenyewe na baba wa Mjerumani.

Rüdiger alicheza mechi yake ya kwanza ya Bundesliga akiwa na Stuttgart mnamo Januari 19, 2012 akiwa na umri wa miaka 18.

Baada ya muda mrefu kwenye Bundesliga, beki huyo alisajiliwa na Roma mwaka 2015 na kucheza ligi ya Serie A hadi 2017, alipojiunga na Ligi ya Uingereza kufuatia kuhamia Chelsea.

Nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Real Madrid, Antonio Rüdiger amejiimarisha tangu alipowasili katika klabu hiyo ya Uhispania majira ya joto ya 2022.

Rüdiger ni mchezaji muhimu katika timu ya taifa ya Ujerumani na alicheza kwa mara ya kwanza mwaka 2014. Na ameicheza mechi 68.

Ametoka kushinda Champions League mara ya pili (baada ya taji la kwanza akiwa na Chelsea 2021).

Nathan Aké (Uholanzi - Ivory Coast)

Alizaliwa Februari 18, 1995 na baba kutoka Ivory Coast na mama kutoka Uholanzi, Nathan Benjamin Aké alicheza katika timu zote za vijana za Uholanzi.

Ni beki wa kati, amecheza mechi 13 akiwa na kikosi cha kwanza cha Uholanzi. Pia ni beki wa klabu ya Manchester City.

Shirikisho la soka laIvory Coast na kocha wa zamani wa The Elephants, Marc Wilmots, walijaribu kumshawishi ajiunge na Ivory Coast 2017. Lakini mchezaji huyo ambaye alikuwa akichezea klabu ya Bournemouth wakati huo, alikataa.

Manuel Akanji (Sweden - Nigeria)

Maelezo ya picha,Manuel Akanji wakati wa mechi ya kufuzu UEFA EURO 2024 kati ya Sweden na Belarus Oktoba 15, 2023 huko St Gallen, Sweden.

Alizaliwa Julai 19, 1995 huko Neftenbach, Sweden na baba Mnigeria, Manuel Akanji alicheza mechi yake ya kwanza na Sweden, dhidi ya Visiwa vya Faroe Juni 9, 2017.

Amepitia Borussia Dortmund, Akanji alisajiliwa na mabingwa wa Uingereza Manchester City katika msimu wa 2022. Wakati wa msimu 2022-2023, alitwaa ubingwa wa England, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa.

Jules Koundé (Ufaransa – Benin)

Amezaliwa wa mama wa Ufaransa na baba wa Benin, Jules Koundé ni beki hodari katika ligi ya Uhispania tangu 2019, alicheza Sevilla FC kisha Barcelona tangu Juni 2022.

Akiwa na umri wa miaka 25, mchezaji huyo ambaye bado ana familia nchini Benin, ameitwa katika timu ya Ufaransa tangu 2021.

Wakati wa Kombe la Dunia la 2022, Jules Koundé alicheza kama mlinzi wa kati, alianza mashindano kwenye benchi, kabla ya kuchukua nafasi ya Didier Deschamps kama beki wa kulia. Ni nafasi ambayo anaichezea klabu yake ya FC Barcelona.

N'Golo Kanté (Ufaransa - Mali)

N'Golo Kanté anasifika kwa ustahimilivu wake, uwezo wake wa kurejesha mipira, unyenyekevu wake na ari yake.

Mali ni nchi ya wazazi wake. Kiungo huyo wa kati wa Ufaransa aliitwa kwa mara ya kwanza na timu ya Ufaransa Machi 17, 2016.

Kanté alicheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa katika Uwanja wa Stade Malherbe mjini Caen, kabla ya kung'ara kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, akiwa na Leicester City kisha Chelsea.

Juni 2023 Mfaransa huyo aliondoka Chelsea baada ya miaka 7 katika klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Saudi ya Al-Ittihad.

Kwa mara ya kwanza tangu aondoke Chelsea katika msimu wa joto wa 2023 na uhamisho wake kwenda Saudi Arabia, N'Golo Kanté, anayechezea klabu ya Al-Ittihad, ameitwa kwenye timu ya Ufaransa kucheza Euro 2024. Akiwa na umri wa miaka 33.

Denis Zakaria (Sweden - Sudan Kusini/Congo)

Denis Zakaria, 26, alizaliwa huko Geneva na mama kutoka Sudan Kusini na baba wa Congo. Angeweza kuchezea moja ya nchi hizi mbili, lakini chaguo lake likawa Sweden, nchi yake ya kuzaliwa.

Akiwa na umri wa miaka 17 tu, alicheza mechi yake ya kwanza Novemba 2014, dhidi ya FC Lausanne-Sport. Kwa uwezo wake mkubwa, mwaka uliofuata 2015, alisajiliwa na Bern.

Katika msimu wa joto wa 2017, akiwa na umri wa miaka 21, Denis Zakaria aliondoka nchi yake ya asili na kujiunga na Bundesliga na Borussia Mönchengladbach.

Baada ya miaka mitano kukaa Ujerumani, alijiunga na Juventus Turin wakati wa dirisha la msimu wa baridi wa 2022 katika ligi ya Serie A na kushiriki Ligi ya Mabingwa.

Kisha alitolewa kwa mkopo kwenda Chelsea (alikocheza mechi 11, bao 1) wakati wa msimu wa 2022-2023, kisha akasaini mkataba wa misimu mitano Agosti 2023 na AS Monaco.

Aliwakilisha nchi yake katika mashindano makubwa manne ya mwisho ya kimataifa (Mashindano ya Ulaya ya 2016 na 2020 na Kombe la Dunia la 2018 na 2022).

Denis Zakaria, daima amethibitisha kushikamana na ukoo wake wa Kiafrika, husafiri hadi DRC kwenda kijiji cha mama yake, na huko Sudan Kusini, na huzungumza lugha zake za asili.

Leroy Sane (Ujerumani - Senegal)

Mtoto wa mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Senegal Souleymane Sané. Mwanawe Leroy Sané ameamua kuichezea Ujerumani mwaka 2015.

Winga wa Bayern Munich, alikuwa kwenye vitabu vya Shirikisho la Soka la Senegal, angeweza kufuata nyayo za baba yake na kutetea rangi za Simba wa Teranga.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, jina lake la kwanza ni heshima kwa Claude Le Roy, kocha wa zamani wa Senegal.

Leroy Sané, hajacheza mechi na timu ya Ujerumani tangu Novemba 2023, alitangaza kuwa yuko tayari kuichezea Ujerumani.

Jumatatu Juni 3, Wajerumani walitoka sare (0-0) na Ukraine. Leroy Sané hakucheza kwani alikuwa bado anatumikia adhabu ya kutocheza mechi tatu.

Mechi dhidi ya Ugiriki mjini Mönchengladbach ni mazoezi ya mwisho ya Ujerumani kabla ya mechi yao ya kwanza ya Euro dhidi ya Scotland Juni 14.

Winga wa Bayern Munich aliyewahi kuichezea Manchester City. Kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann alimwita Sané katika kikosi chake.

Bukayo Saka (Nigeria – Englanda)

Amezaliwa katika vitongoji vya London na wazazi wa Nigeria na aliwahi kuombwa na Shirikisho la Soka la Nigeria kujiunga na Super Eagles, winga huyo wa Arsenal anajiandaa kushiriki michuano ya Ulaya kwa mara ya pili.

Ni mchezaji wa kimataifa wa Uingereza tangu Oktoba 2020, Bukayo Saka alicheza mechi yake ya kwanza katika timu ya taifa ya Uingereza Novemba 2020.

Bukayo Saka anasema kuzaliwa na kukulia nchini Uingereza kulimzuia kuchagua timu ya taifa ya Nigeria. Alisema, ingekuwa vigumu kuchagua Nigeria kutokana na mazingira yake binafsi aliyokulia.

“Familia yangu yote imekuwa ikiishi Uingereza siku zote, itakuwa ngumu sana kwangu kuzoea mazingira ambayo sijawahi kuyapitia tangu utoto wangu,” alisema.

Ameichezea Uingereza katika timu za vijana ya chini ya umri wa 16, 17, 18, 19 na 21. Mshambuliaji huyo alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Uingereza 2022 na 2023.

Romelu Lukaku (Ubelgiji – DRC)

Maelezo ya picha,Mshambulizi nyota wa Ubelgiji mwenye asili ya Congo, Romelu Lukaku

Romelu Lukaku alizaliwa Mei 13, 1993 huko Antwerp, mji wa bandari nchini Ubelgiji, na wazazi wa Ubelgiji-Congo.

Alianza kucheza kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16 akiwa na klabu yake ya mazoezi ya Anderlecht, ambayo ilimfanya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza Ligi ya Mabingwa akiwa na klabu hiyo ya Ubelgiji.

Katika msimu wake wa pili wa kulipwa, 2009-2010, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alimaliza mfungaji bora katika ligi ya Ubelgiji.

Mwaka 2011, alijiunga na Ligi ya Uingereza kwa kusajiliwa na Chelsea lakini baadaye akatolewa kwa mkopo Kwenda West Bromwich na kufunga mabao 17 katika mechi 35 za ligi.

Lukaku aliendelea na maisha yake Uingereza kwa kucheza Everton kisha miaka miwili kucheza Manchester United. Mwaka 2021, aliondoka Uingereza na kujiunga na ligi ya Serie A ya Italia akichezea Inter Milan ambapo alijaza mabao na kushinda taji na Nerra Zurri.

Sasa ni mchezaji wa AS Roma, Romelu Lukaku yuko katika nafasi ya juu ya wafungaji katika wa timu ya taifa ya Ubelgiji.

Kylian Mbappé (Ufaransa – Cameroon)

Maelezo ya picha,Kylian Mbappé alizaliwa na baba wa Cameroon na mama wa Algeria.

Bila shaka ni mmoja wa nyota wa michuano hii ya Ulaya 2024. Kylian Mbappé amesajiliwa na Real Madrid hivi karibuni, siku chache kabla ya kuanza kwa Euro 2024.

Alizaliwa na baba kutoka Cameroon na mama wa Algeria, Kylian Mbappé alifanya chaguo la kuvaa jezi ya Ufaransa 2017 akiwa na umri wa miaka 18.

Akiwa na umri wa miaka 25, baada ya misimu saba huko Paris Saint-Germain, tayari amepata mafanikio ya ajabu.

Mfungaji bora wa michuano ya kombe la dunia nchini Qatar 202, amepata mataji kadhaa akichezea ligi ya Ligue 1, Mbappé tayari ana rekodi kubwa katika soka.

Alipoulizwa kuhusu ugumu wa kutwaa ubingwa wa Ulaya, mchezaji huyo mpya wa Real Madrid alisema, ni vigumu zaidi kushinda kombe la mataifa ya Ulaya kuliko Kombe la Dunia.

Akiteuliwa kuwa nahodha baada ya Kombe la Dunia la 2022. Atawaongoza wachezaji wenzake kwenye kombe la Ulaya, akiwa katika maisha yake ya ujana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved