logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Enzo Fernandez aongoza orodha ya jezi za Chelsea zilizonunuliwa zaidi msimu uliopita

Nambari ya tatu ilishikiliwa na mkongwe Thiago Silva na jezi yake nambari 6 mgongoni,

image
na Davis Ojiambo

Michezo04 July 2024 - 09:32

Muhtasari


  • • Winga wa Ukraine Mykhailo Mudyryk alishika nafasi ya 5 katika mauzo ya jezi yake yenye nambari 10 mgongoni.
  • • Sajili mpya ambaye pia alikuwa mfungaji bora kwa klabu hiyo, Cole Palmer akishika nafasi ya nne kwa mauzo ya jezi yake ya nambari 20 mgongoni.
Wachezaji wa Chelsea waliouza jezi nyingi

 Miamba wa soka kutoka London nchini Ungereza, Chelsea maarufu kama The Blues wametoa takwimu za jinsi jezi za wachezaji wao mbalimbali zilivyonunuliwa sokoni na mashabiki na wapenzi wa Chelsea.

Katika takwimu hiyo, Chelsea walitoa orodha ya wachezaji 5 wa kwanza ambao jezi zao zilikuwa zinanunuliwa sokoni bila kukawia.

Winga wa Ukraine Mykhailo Mudyryk alishika nafasi ya 5 katika mauzo ya jezi yake yenye nambari 10 mgongoni huku sajili mpya ambaye pia alikuwa mfungaji bora kwa klabu hiyo, Cole Palmer akishika nafasi ya nne kwa mauzo ya jezi yake ya nambari 20 mgongoni.

Nambari ya tatu ilishikiliwa na mkongwe Thiago Silva na jezi yake nambari 6 mgongoni, ambaye alifanya kazi kubwa kuhimiza klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa jedwali.

Silva, 39, ambaye aliondoka kishujaa mwishoni mwa msimu alimiminiwa sifa kwa kuonyesha uongozi na uzoefu wake kwa timu hiyo ambayo ilikuwa na asilimia kubwa ya wachezaji wachanga chini ya umri wa miaka 25.

Nafasi ya pili ilishikiliwa na nahodha Reece James ambaye jezi yake ya nambari 24 mgongoni iliwavutia wengi licha ya kutumikia karibia msimu wote akiwa nje kutokana na jeraha.

James alirejea mwishoni mwa msimu na kushiriki mechi mbili kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu ambayo itamfungia mechi 4 za ufunguzi wa msimu ujao wa mwaka 2024/25.

Katika nafasi ya kwanza, kiungo wa kati Muargentina Enzo Fernandez aliongoza kwa mauzo mengi ya jezi yake nambari 8 mgongoni.

Licha ya kusuasua kwa baadhi ya mechi, Enzo Fernandez bado anachukuliwa kama moja ya hazina kuu na yenye thamani kwa klabu ya Chelsea na anatarajiwa kuipata fomu yake nzuri chini ya kocha mpya Enzo Maresca msimu huu.

Chelsea walifaulu katika kumshawishi Enzo Fernandez kutoshiriki mechi za Oimpiki na timu ya taifa la Argentina ambazo zitang’oa nanga mwezi kesho nchini Ufaransa.

Lengo lao lilikuwa kwamba Fernandez awe mmoja wa wachezaji ambao wataanza mazoezi na mechi za kujifua kuelekea msimu mpya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved