logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Man United kuwafuta kazi wafanyakazi 250

lengo ni kupunguza idadi ya watu na gharama za wafanyikazi. United ina wafanyikazi wa kudumu 1,150.

image
na Davis Ojiambo

Michezo04 July 2024 - 04:46

Muhtasari


  • • Vyanzo vya klabu sasa vinasema mabadiliko makubwa ya kifedha yanahitajika ili kukomesha kupanda kwa gharama za mwaka hadi mwaka.

Manchester United itapunguza kazi 250 kama sehemu ya kupunguza gharama na kufutilia mbli baadhi ya shughuli "zisizo muhimu".

Mkurugenzi wa United Sir Dave Brailsford ameongoza mapitio makubwa ya uendeshaji wa klabu tangu umiliki wa Inoes wa klabu hiyo kuthibitishwa mwezi Desemba.

Sir Jim Ratcliffe alikuwa tayari amewaambia wafanyikazi juu ya hamu yake ya wao kurudi kufanya kazi katika maeneo ya uwanja wa klabu.

Hata hivyo, vyanzo vya klabu sasa vinasema mabadiliko makubwa ya kifedha yanahitajika ili kukomesha kupanda kwa gharama za mwaka hadi mwaka.

Tathmini hiyo imehitimishwa, kulingana na muundo, ukubwa na kwamba sura ya klabu haionyeshi uchezaji wa sasa na wana wafanyakazi wengi kuliko wanaohitaji.

Vyanzo vinasema uokoaji wa gharama umetambuliwa karibu na shughuli "zisizo muhimu", ambazo zitakoma.

Bado haijafafanuliwa ni shughuli gani hizi, lakini lengo ni kupunguza idadi ya watu na gharama za wafanyikazi. United ina wafanyikazi wa kudumu 1,150.

Mtendaji mkuu wa muda Jean-Claude Blanc aliwasilisha habari za kupunguzwa kwa wafanyikazi katika mkutano wa wafanyikazi na karibu watu 800 waliohudhuria.

Hatua hiyo inaelekea kupokewa vibaya, huku wengi wakitaja usajili duni kwenye kikosi cha kwanza kwamba umepoteza pesa nyingi zaidi kuliko zitakazookolewa kwa kupunguza wafanyikazi .

Man Utd imemthibitisha Ashworth kama mkurugenzi wa michezo


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved