logo

NOW ON AIR

Listen in Live

West Ham wapo kwenye mazungumzo ya kumrejesha N’Golo Kante EPL

Kante alionyesha mchezo wa kupendeza wakati wa mashindano ya Euro 2024.

image
na Davis Ojiambo

Michezo19 July 2024 - 13:19

Muhtasari


  • •West Ham wanaamini kuwa uzoefu uliodhihirisha na Ngolo Kante kwenye mashindano ya Euro 2024 utawasaidia.
  • •Kiungo mkabaji,Kalvin Phillips hajaonyesha ubora tangu kujiunga na West Ham kwa mkopo kutoka Manchester City.
Ngolo Kante

West Ham wanatumai kumsajili kiungo wa zamani wa Chelsea N’Golo Kanté kutoka Al-Ittihad kwa kiasi cha pauni milioni 20.

Kulingana na gazeti la The Guradian;mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanaendelea na kuna nia ya kufanya makubaliano kwa pande zote mbili kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye aliichezea Ufaransa kwenye Euro 2024.

Kanté, ambaye alihamia Saudi Arabia mnamo 2023 baada ya miaka saba na Chelsea, alithibitisha katika Euro 2024 kwamba bado ana uwezo wa kuimarika kwa kiwango cha juu zaidi.

The Hammers wana hamu ya kusajili kiungo mkabaji baada ya Kalvin Phillips kutotimiza matarajio wakati wa kipindi cha mkopo kutoka Manchester City msimu uliopita na dili lake halijakamilika.

Meneja wao mpya, Julen Lopetegui, amekuwa akivutiwa na Kanté kwa muda mrefu na alitaka kumsajili kiungo huyo katika kipindi kifupi cha kuinoa Real Madrid. Hapo awali West Ham walikuwa wakimtaka kiungo wa kati wa Uhispania Aleix García lakini akachagua kujiunga na mabingwa wa Bundesliga Bayer Leverkusen.

Kiungo huyo, ambaye ameichezea nchi yake mechi 61, alicheza katika mechi zote sita za Ufaransa kwenye Euro 2024 .

Katika ngazi ya kimataifa alishinda kombe la dunia la 2018 na West Ham wanaamini kwamba mtu wa uzoefu wake atakuwa muhimu katika enzi yao mpya chini ya Lopetegui, ambaye alichukua nafasi ya David Moyes mwishoni mwa msimu uliopita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved