Mancini alikuwa ameteuliwa kuwa kocha mkuu kwa kandarasi ya miaka minne Agosti mwaka jana, na mkataba huo ukiwa na thamani ya pauni milioni 21 kwa mwaka.
Uteuzi wake ulikuja wiki chache baada ya kujiuzulu kama meneja wa Italia, ambapo hapo awali alikuwa ameiongoza timu ya taifa kutwaa ubingwa wa Uropa mwaka 2021.
Shirikisho la Soka la Saudi Arabia lilisema kuwa 'makubaliano ya pamoja' yamefikiwa kumaliza mkataba wa Mancini.
Habari hizo zilifuatia uvumi katika siku za hivi karibuni kwamba shirika hilo lilikuwa tayari kumfuta kazi Muitaliano huyo.
"Bodi ya Wakurugenzi ya Shirikisho la Soka la Saudia na kocha wa timu ya taifa, Muitaliano Roberto Mancini, walifikia makubaliano ya pamoja leo ambayo ni pamoja na kusitisha uhusiano wa kimkataba," ilisema taarifa.
'Baraza linatoa shukrani zake kwa Bw. Roberto Mancini, akimtakia mafanikio mema katika kazi yake hiyo.
'Bodi ya Wakurugenzi inathibitisha kwamba jina la kocha ajaye wa timu ya taifa litatangazwa siku chache zijazo baada ya kukamilika kwa taratibu za kandarasi.'
Mancini anaondoka Saudi Arabia na taifa hilo likiwa katika nafasi ya tatu katika Kundi C la raundi ya tatu ya mchujo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 kwa bara la Asia.
Mbili za juu katika kundi hilo zitafuzu moja kwa moja kwa Kombe la Dunia, huku timu za tatu na nne zikisonga mbele hadi raundi ya nne ya mchakato wa kufuzu.
Saudi Arabia wako sawa kwa pointi na Australia walio nafasi ya pili baada ya kushinda moja, sare mbili na kushindwa moja katika mechi zao nne za mwanzo.
Mapema mwezi huu, Mancini alionekana akizozana na kundi la wafuasi wake kufuatia sare ya 0-0 ya Saudi Arabia na Bahrain.
Matokeo hayo yameongeza mwendo wa ushindi mmoja katika mechi tano. Mancini pia alikuwa amezungumza dhidi ya athari za uwekezaji wa Saudi Pro League katika vipaji vya ng'ambo, ikiwa ni pamoja na Cristiano Ronaldo.
Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 59 alidai kuingia kwa wachezaji wapya kumeathiri vibaya timu ya taifa.