Kampuni ya kutengeneza mavazi ya Adidas imezindua kiatu chenye sahihi ya mchezajikinda wa Barcelona Lamine Yamal kama njia ya kusherehekea ufanisi wa mwanasoka huyo.
Uzinduzi wa kiatu hicho kinatokana na kuhitimu kwa Yamala katika shule ya upili na kufika kileleta kwa mashindanoya UEFA EURO ambapo timu yake ya taifa la Uhispania ilitinga fainali ya mashindano hayo.
Kiatu hicho kilichotengenezwa na kampuni ya Adidas kina sifa za kuvutia macho kutokana na ustadi uliotumika kukitengeneza kikiashiria ubora wa mchezaji huyo aliyetajwa kuwa bora wa chini wa umri wa miaka 21 barani Ulaya mwaka 2024.
Katika mwenokano wa kiatu hicho, Lamine alichagua rangi ya zambarau ambao ni mojawapo wa rangi anazozipenda ila nembo F50 kwenye ngozi ya kiatu hicho ikibadilishwa na tarakimu tatu za mwisho za nembo ya nambari za posta wa mji wa nyumbani anakotoka Yamal ambayo ni 304 iliyoandikwa kwa rangi ya dhahabu. Mwonekano huo umetumika kuonyesha heshima kwa jamii ambayo imemtazama akiwa mtoto mchanga mpaka akibadilika na kuwa kipaji cha kizazi.
Akiongea kuhusu ushirikiano wake na Kampuni ya Adidas Lamine alisema kuwa tukio hilo limekuwa kama ndoto kwa maisha yake.
"Mwaka huu umekuwa kama ndoto kwangu, na kufanya kazi na adidas kwenye kiatu changu cha kwanza iliyosainiwa imekuwa nzuri sana. Waliponialika kufanya kazi na wabunifu na kuwa miongoni mwa walioiunda kiatu hicho, nilifurahi sana kuona jinsi ilivyoundwa,’’ Alisema Lamine
Adidas walisherehekea uzinduzi huo kwa kupiga picha maalum huku Lamine Yamal akiwa amevalia mavazi ya rangi ya waridi ya kuhitimu. Lamine alikiri kuwa anapenda rangi ya pinki.
‘’Pinki ni mojawapo ya rangi ninazozipenda, na mimi ni mchezaji ambaye hupenda kuleta umaridadi uwanjani, kwa hivyo ilikuwa muhimu kwangu kwamba rangi hilo litumike,’’ Aliongezea Yamal.
Sam Handy, Meneja Mkuu wa Soka katika Kampuni wa Adidas, alisema kuwa ni vigumu kwa wachezaji wengi kuwa miongoni mwa wale wanaoshirikiana katika shughuli kama hiyo.
"Tunapozungumzia wachezaji ambao wana saini zao za kiatu cha adidas, tunaangalia majina machache tu ambayo yamefikia kiwango hicho cha uwezo na umaarufu,’’ Alisema Handy.
Ikiwa ni jozi 304 pekee zinazopatikana kununua duniani kote, kifurushi cha adidas F50 LY304 kinaweza kununuliwa kuanzia Desemba 18.