Skauti wa zamani wa Real Madrid Manolo Romero amemuonya Vinicius Junior kwamba rais wa klabu hiyo Florentino Perez atamuuza huku akimpendelea Kylian Mbappe kuliko Mbrazil huyo.
Hatimaye Perez alipata nafasi ya kukamilisha ndoto yake ya kumsajili Mbappe katika majira ya joto baada ya mkataba wa Mfaransa huyo kuisha huko Paris Saint-Germain.
Hata hivyo, usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ulionekana kuwa hauhitajiki huku Vinicius na Rodrygo wakiwa wametulia katika shambulizi moja bora zaidi duniani.
Mbappe amekuwa na wakati mgumu kuonyesha kiwango chake bora kwa Real Madrid baada ya kuhamia Santiago Bernabeu huku akilazimika kucheza katikati ya safu ya ushambuliaji huku Vinicius akimiliki winga ya kushoto inayopendekezwa.
Skauti wa zamani wa Real Madrid Romero anasema kwamba Perez angemuuza Vinicius ikiwa bei yake ni sawa kwani Mbappe ndiye "kipenzi" cha mkuu wa klabu.
Akiongea na SPORT, Romero alisema: “Nilikuwa na hakika kwamba [Vinicius] angeondoka. Wakija na zaidi ya Euro 300 milioni (Sh40.5 bilioni), nina uhakika kuwa Florentino atamuuza, hata anampeleka uwanja wa ndege kwa gari lake.
"Jambo ni kwamba €300 milioni (..ni pesa nyingi. Nadhani kipenzi cha Florentino atakuwa Mbappe. Amekuwa nyuma yake kwa miaka saba."
Mbrazil huyo amekuwa akihusishwa pakubwa na kuhamia Saudi Pro League. Hata hivyo, inaonekana ni vigumu kuondoka Ulaya wakati bado yuko katika ubora wake.