Winga wa Manchnester United Amad Diallo ametia sahihi mkataba mpya na miamba hao wa soka wa jiji la Manchester wa miaka mitano na nusu. Mkataba huo utamfikisha hadi mwaka wa 2030 mwezi Juni.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Ivory Coast ameelezea furaha ya kuwepo kwa mkataba mpya na Man United. Mkataba wa awali ulikuwa unakaribia kikomo ambapo unakamilika mwisoni mwa msimu huu.
Diallo amekuwa kwenye ubora tangu tangu kujiunga na klabu hiyo mnamo mwaka wa 2021 akiwa amefunga mabao tisa katika mechi 50 alizoshiriki.
"Ninajivunia kusaini mkataba huu mpya. Nimekuwa na nyakati za ajabu na klabu hii tayari lakini kuna mengi zaidi yanakuja," Alisema Diallo baada ya kutia sahihi mkataba huo mpya.
Katika malengo yake baada ya kutia sahihi mkataba huo mpya, Diallo amesema kwamba ana matumaini ya kuandikisha historia katika klabu hiyo kwenye miaka atakayokuwa anatumikia klabu hiyo.
Vile vile, amekiri kuwa Manchester United inakabiliwa na wakati mgumu haswa msimu huu akiadhidi kujitolea kuisaidias kurejesha adhi ya timu hiyo.
"Nina matarajio makubwa kwenye mchezo na ninataka kuweka historia katika Manchester United. Umekuwa msimu mgumu kwa kila mtu, lakini ninaamini kabisa kwamba tuko kwenye njia sahihi na siku zijazo zitakuwa nzuri. Niko tayari kutoa kila kitu kusaidia timu na kuwafanya mashabiki wetu wajivunie tena." Aliongeza Diallo.
Fomu ya Amad Diallo imekuwa njema huku hivi karibuni akisaidia Man United kupata bao muhimu la kusawazisha kwenye mechi ya ligi dhidi ya Liverpool.
Diallo alisalia kambini Old Trafford wakati wa kocha
aliyetimuliwa Erik Ten Hag wakati ambapo kulikuwepo na uwezekano wa kuondoka
msimu uliopita.