GWIJI wa mchezo wa kandanda, Cristiano Ronaldo amefichua kwamba hakuna klabu alichofurahia Maisha yake ya kandanda Zaidi kuliko Real Madrid.
Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa
kurejea Real Madrid, na mwandishi wa habari wa Uhispania Eduardo Aguirre,
Ronaldo alisema: "Labda baada ya kumaliza kazi yangu, kitu kinaweza
kutokea."
Akitafakari juu ya wakati wake nchini
Uhispania, mshambuliaji huyo mkongwe alielezea kama kilele cha safari yake ya
kikazi.
"Kipindi changu Real
Madrid ndicho cha furaha zaidi kwangu katika masuala ya soka,"
alikiri, akisisitiza nafasi maalum ambayo klabu inashikilia moyoni mwake.
Mkataba uliopo wa Ronaldo na Al-Nassr,
ambao unaripotiwa kumuingizia takriban pauni milioni 3.1 kwa wiki, unatarajiwa
kuisha msimu huu wa joto.
Hata hivyo, ripoti zimeonyesha kuwa
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 tayari amekubali kuendelea na klabu hiyo
ya Saudi Pro League, huku kandarasi mpya ikikadiriwa kuwa na thamani ya euro
milioni 183 (£154m/$188m) kila mwaka, sawa na €15 milioni (£12.6m/$15m) kwa
mwezi au €3.8 milioni kwa wiki.
Licha ya kukaribia mwisho wa maisha yake ya
soka, Ronaldo anaendelea kuwa na malengo makubwa na supastaa huyo wa zamani wa
Manchester United alishawahi kusema kwamba kustaafu sio ajenda yake ya haraka,
akiwa na lengo la kibinafsi la kufikisha mabao 1,000 kabla ya kutaja wakati
wake wa kucheza.
Kusaka rekodi zake bila kuchoka kuliendelea
katika ushindi wa hivi majuzi wa Al-Nassr wa 3-1 dhidi ya Al-Fateh, ambapo
alipata bao tena, na kufikisha mabao 920 katika maisha yake ya soka.
Ronaldo alitumia
kipindi cha miaka 9 Real Madrid kati ya 009 hadi 2018 ambapo alicheza jumla ya
mechi 292 na kufunga mabao 311.