logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Manchester City Yakutanishwa Na Real Madrid Kwenye Hatua Ya Muondoano

Mechi hizo zitachezwa kwa awamu mbili – nyumbani na Ugenini na City watakuwa wa kwanza kuwakaribisha Real nchini Uingereza kabla ya kusafiri nchini Uhispania.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Michezo31 January 2025 - 15:07

Muhtasari


  • Mechi hizo zinatarajiwa kuanza Februari 11 na kuendelea hadi fainali mwezi Mei.
  • Droo ya awamu ya muondoano ya hatua ya mtoano ya UEFA 2024/25 ilithibitishwa saa chache adhuhuri.



VILABU 16 vya vinavyowania nafasi 8 za kutinga hatua ya 16 bora vimejua hatima yao adhuhuri ya leo hii Ijumaa ya Januari 31.

Droo ya awamu ya muondoano ya hatua ya mtoano ya UEFA 2024/25 ilithibitishwa saa chache adhuhuri.


Timu zitakazoshiriki hatua ya mtoano ni: Atalanta, Borussia Dortmund, Real Madrid, Bayern Munich, Milan, PSV, Paris Saint-Germain, Benfica, Monaco, Brest, Feyenoord, Juventus, Celtic, Manchester City, Sporting CP na Club Brugge.


Hii hapa orodha kamili ya mechi za mchujo kwa awamu ya muondoano ya Ligi ya Mabingwa kwa wanaume, kufuatia droo hiyo.


Mechi hizo zitachezwa kwa awamu mbili – nyumbani na Ugenini na City watakuwa wa kwanza kuwakaribisha Real nchini Uingereza kabla ya kusafiri nchini Uhispania.


Hii hapa orodha kamili ya mechi ya awamu ya muondoano;


·         Manchester City (ENG) vs Real Madrid (ESP)


·         Celtic (SCO) dhidi ya Bayern Munich (GER)


·         Club Brugge (BEL) dhidi ya Atalanta (ITA)


·         Sporting CP (POR) dhidi ya Borussia Dortmund (GER)


·         Juventus (ITA) dhidi ya PSV (NED)


·         Feyenoord (NED) dhidi ya AC Milan (ITA)


·         Brest (FRA) dhidi ya Paris Saint-Germain (FRA)


·         AS Monaco (FRA) dhidi ya Benfica (POR)


Mechi hizo zinatarajiwa kuanza Februari 11 na kuendelea hadi fainali mwezi Mei.


Hizi hap ani tarehe za ratiba za mechi hizo;


·         11-12 Februari 2025: Mchujo wa awamu ya muondoano wa mtoano, mkondo wa kwanza


·         18-19 Februari 2025: Mchujo wa awamu ya muondoano wa mtoano, mkondo wa pili


·         4-5 Machi 2025: Raundi ya 16, mkondo wa kwanza


·         11-12 Machi 2025: Raundi ya 16, mkondo wa pili


·         8-9 Aprili 2025: Robo-fainali, mkondo wa kwanza


·         15-16 Aprili 2025: Robo-fainali, mkondo wa pili


·         29-30 Aprili 2025: Nusu fainali, mkondo wa kwanza


·         6-7 Mei 2025: Nusu fainali, mkondo wa pili


·         Tarehe 31 Mei 2025: Fainali



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved