
Liverpool itacheza na Paris Saint-Germain katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa huku Arsenal ikimenyana na PSV Eindhoven na Aston Villa kumenyana na Club Brugge.
Mechi za hatua ya 16 bora zitafanyika Machi 4 na 5 huku
mechi za mkondo wa pili zikichezwa Machi 11 na 12.
Timu zote tatu za Uingereza
ziko upande mmoja wa droo hiyo ikimaanisha kuwa Liverpool wanaweza kukutana na
Aston Villa katika robo fainali kisha Arsenal katika nusu fainali.
Klabu yoyote ya Uingereza
inayotarajia kutinga fainali inaweza kukutana na mabingwa Real Madrid lakini
hawatacheza na Barcelona hadi fainali.
Liverpool walimaliza kileleni mwa awamu ya ligi huku PSG
wakifuzu kupitia hatua ya mtoano kwa ushindi wa kushangaza wa 10-0 dhidi ya
Brest.
Arsenal walifanikiwa kufuzu katika mechi ya tatu wakitoka
sare ya bila kufungana dhidi ya PSV, ambao waliwatoa Juventus kwenye mechi ya
mtoano kwa ushindi wa 3-1 wa mkondo wa pili na kushinda kwa jumla ya 4-3.
Aston Villa ilinyakua nafasi ya mwisho ya kufuzu moja kwa
moja na sasa itamenyana na Club Brugge baada ya kuishinda Atalanta kwa ushindi
wa jumla wa 5-2.
Hii hapa droo kamili ya mechi hizo;
1.
Borussia Dortmund dhidi ya Lille
2.
Real Madrid vs Atletico Madrid
3.
Bayern Munich vs Bayer Leverkusen
4.
PSV Eindhoven vs Arsenal
5.
Feyenoord dhidi ya Inter Milan
6.
Paris Saint-Germain vs Liverpool
7.
Benfica vs Barcelona