
KOCHA wa Chelsea ametania sababu ya kipa Robert Sanchez kunyoa na kuwa kipara.
Akizungumza Ijumaa wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari kuelekea safari ya Kwenda Villa Park katika pambano la ligi
ya Premia, Enzo Maresca alitania kwamba yeye ndiye aliyemtaka Sanchez kunyoa
kipara.
Muitaliano huyo alisema kwamba alimwambia
kipa huyo wa Uhispania kunyoa kipara ikiwa alikuwa anataka kurejeshewa nafasi
yake ya kucheza kama golikipa nambari moja.
"Nilimwambia 'ikiwa unataka kucheza
tena, unahitaji kukata nywele sawa na mimi,” Maresca alisema huku akicheka.
Sanchez alishushwa hadi kipa wa akiba
kwenye benchi na nafasi yake kuchukuliwa na raia wa Denmark Filip Jorgensen
ambaye awali alikuwa akichezeshwa kwenye mechi za Conference, FA na Carabao.
Aidha, Enzo Maresca alikiri morali ndani ya
kambi ya Chelsea iko chini na kwamba wachezaji wake 'wamefadhaika'.
The Blues wameshinda mara mbili pekee
katika mechi zao tisa za mwisho za Ligi ya Premia na matumaini yao ya kufuzu
kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao yapo kwenye mizani.
Wameshuka kutoka nafasi ya pili kwenye
jedwali hadi nafasi ya sita nyuma ya Manchester City na Bournemouth, jambo
ambalo limeongeza presha kwa Maresca baada ya kuanza vyema msimu huu.
Kabla ya mchuano mkali na Aston Villa siku
ya Jumamosi, Muitaliano huyo alikataa kuficha ukweli kwamba wachezaji wake
hawafurahishwi na hali ya sasa.
"Roho ya timu kwa wakati huu inabidi
ifadhaike, katika suala hili lazima wasumbuke," Maresca alisema.
“Tunapaswa kukasirika kwa sababu
hatujafurahishwa na matokeo.
"Sote tunafahamu tuko katika klabu
ambayo hatuko hapa ili kunusurika, lakini kupigania kushinda mataji. Ni
wachezaji wale wale ambao kwa mechi 19-20 walikuwa [katika] nne bora, wa pili
kwa sehemu kubwa ya msimu.
"Kwa hakika, baada ya muda huu,
watakuwa wachezaji bora na wataalamu bora."
Chelsea imekabiliwa na majeraha kwa
wachezaji muhimu, ikiwapoteza Wesley Fofana na Benoit Badiashile kwa wakati
mmoja kabla ya Mwaka Mpya. Romeo Lavia pia hajatoka nje ya uwanja tangu Desemba
na anaendelea kukosekana.
Hivi majuzi, Maresca amelazimika
kukabiliana na pigo mara mbili baada ya Noni Madueke na Nicolas Jackson
kutengwa kwa wiki kadhaa. Na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 45 alipendekeza
kupoteza kwa wachezaji hao kumekuwa sababu ya kupungua kwao.