
KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amefichua kwamba nyota wake Cole Palmer alishiriki katika mchezo wa premia dhidi ya Leicester City akiwa hajisikii vizuri kiafya.
Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya
mechi baada ya ushindi mwembamba wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Leicester
City kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Muitaliano huyo alisema kwamba Palmer
hakushiriki mazoezi siku mbili kabla ya siku ya mechi.
Hata hivyo, licha ya kutoshiriki mazoezi
kutokana na hali yake ya kuendesha, Maresca alisema kwamba Palmer aliomba
kujumuishwa kwenye kikosi dhidi ya Leicester.
"Ni rahisi sana: Cole, jana,
hakufanya mazoezi na wakati wa usiku, hakujisikia vizuri. Sababu iliyomfanya
asifanye mazoezi jana ni kwa sababu hakujisikia vizuri. Asubuhi ya leo, aliamka
na akaniuliza, 'Nataka kuwa uwanjani kwa sababu nataka kusaidia timu hii, klabu
hii kucheza Ligi ya Mabingwa'.
"Kwa hiyo katika siku mbili
zilizopita, alikuwa nje kabisa. Homa, ni kitu ninachoweza kusema kwa
Kiingereza? Kuhara. Katika saa 48 zilizopita, hakufanya mazoezi na homa na
hisia hii mbaya. Asubuhi ya leo, aliomba kucheza mchezo na hii inaonyesha jinsi
wachezaji hawa wanataka kuifikisha klabu mahali pake."
The Blues waliwapita Foxes waliokuwa
wakihangaika Jumapili alasiri kutokana na bao zuri la Marc Cucurella dakika ya
60 na ushindi huo ukirejesha timu ya Maresca ndani ya nne bora.
Kocha huyo wa zamani wa Leicester City
aidha alifichua kwamba anahurumia klabu hiyo ambayo sasa huenda ikashushwa Daraja
tena msimu huu baada ya kufanya kazi nzuri ya kuwarejesha kwenye ligi kuu msimu
uliopita.
"Ninawaonea huruma Leicester kwa
sababu nitawashukuru kila mara. Lakini sababu ni kwa sababu ya hili. Wanakuja
hapa wakidhani wanaweza kutushangaza lakini wachezaji walizoea vizuri na hii
ndiyo sababu iliyonifanya kuwa na furaha."
Palmer alikosa kufunga penati yake ya
kwanza katika taaluma yake ya soka na haswa akiwa na klabu ya Chelsea.