
Bingwa mtetezi wa mbio za marathon za Boston Hellen Obiri atakuwa akitetea taji lake leo alasiri.
Obiri, bingwa wa mbio za wanawake 2023 na 2024, analenga kuwa mshindani wa kwanza wa kike kushinda mbio hizo mara tatu mfululizo.
Evans Chebet, mshindi wa mbio za wanaume za Boston Marathon 2022 na 2023, pia atakuwa akiwania ushindi wa tatu katika mbio hizo za World Majors Marathon.
Kundi la wanariadha mashuhuri limekusanywa na waandalizi ili kuwania kitita cha Sh91,420,875 kitakachotunukiwa katika kitengo cha wanaume na wanawake.
Washindi katika vitengo vya wanaume na wanawake watatia kibindoni Sh9,455,000 (dola 150,000), huku mshindi wa pili akiambulia jumla ya Sh9,725,625 (dola 75,000). Wanariadha walioshika nafasi ya tatu wataweka mfukoni Sh5,187,000.
Vilevile kuna bonasi ya rekodi ya Sh6,483,750. WMM ni mfululizo wa mbio saba za marathon kali na za kifahari zaidi ulimwenguni.
Nazo ni Boston Marathon, Tokyo Marathon, London Marathon, Berlin Marathon, Chicago Marathon, New York City Marathon, na Sydney Marathon. Mbio za wanaume zitaanza saa 4:37 (saa za Kenya), na zile za wanawake zitaanza saa 4.47 jioni.
Mashindano yote mawili yatapeperushwa huko Hopkinton, Massachusetts na kuishia kwenye Mtaa wa Boylston.
Chebet, ambaye anafanya mazoezi Kapsabet katika Kaunti ya Nandi chini ya 2Running Athletics Club, anakuja dhidi ya mshindi wa mwaka jana Sisay Lemma wa Ethiopia ambaye alishinda kwa saa mbili, dakika sita na sekunde 17 mbele ya mwenzake Mohamed Esa (2:06:58).
Alimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Lemma na Esa mwaka jana baada ya kukimbia 2:07:22.
Cyprian Kotut, atashiriki katika mbio zake kuu za tatu za marathon, baada ya kumaliza wa tisa mjini Boston mwaka jana na wa pili katika Berlin Marathon mwaka jana. Kotut ni ndugu mdogo wa bingwa wa zamani wa London Marathon Martin Lel.
Wakenya wengine katika mbio za wanaume ni bingwa wa Chicago Marathon John Korir ambaye alikuwa wa nne mjini Boston mwaka jana, na Daniel Mateiko.
Kwa upande wa wanawake, Mkenya Hellen Obiri atakuwa akitafuta kutetea taji lake kwa mwaka wa tatu akikimbia, na kuwa mwanamke wa kwanza kupata ushindi mara tatu mfululizo katika mbio hizo tangu Fatuma Roba mwaka wa 1999.
Obiri atachuana na bingwa mara mbili wa mbio za marathon duniani Edna Kiplagat ambaye alikuwa wa tatu katika mbio za mwaka jana, na Sharon Lokedi aliyemaliza wa pili nyuma yake.
Wanariadha wengine wa Kenya katika mbio za wanawake ni pamoja na Irene Cheptai (2:17:51), Viola Cheptoo (2:22:44) Sharon Cherop (2:22:28), Hellen Obiri (2:23:10), Mary Ngugi (2:20:22), Stacy Ndiwa (2:23:42) na Cynthia 2:25 Limo1).
Baadhi ya washindani kutoka Ethiopia ni pamoja na Amane Beriso (2:14:58), Yalemzerf Yehualaw (2.16:52), Rahma Tusa (2.19:33), na Buze Diriba (2:20:22).