logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chelsea Yashangaza PSG 3-0 Kutwaa Kombe la Dunia la Klabu

Cole Palmer alifunga mabao mawili na kutoa pasi ya bao kwa Joao Pedro.

image
na Tony Mballa

Michezo14 July 2025 - 06:35

Muhtasari


  • Mateso ya PSG yalihitimishwa dakika ya 83 pale Joao Neves alipotolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumvuta nywele Marc Cucurella kwa hasira.
  • Tukio hilo liliibua vurugu kubwa uwanjani mara baada ya mechi kumalizika, huku kocha Luis Enrique akionekana kumpiga Joao Pedro usoni, pamoja na kipa Donnarumma kujihusisha katika tafrani hiyo.

Cole Palmer alionyesha ubora wa hali ya juu katika kipindi cha kwanza huku Chelsea ikiitandika Paris Saint-Germain 3-0 na kutwaa fainali ya Kombe la Dunia la Klabu kwenye Uwanja wa MetLife, New Jersey, siku ya Jumapili.

Kiungo mshambuliaji huyo kutoka Uingereza alifunga mabao mawili na kutoa pasi ya bao kwa Joao Pedro katika mchezo wa mwisho wa mashindano hayo yaliyoandaliwa upya, hali iliyoacha mabingwa wa Ulaya na Ufaransa wakiwa hawana la kujibu kabla ya mapumziko.

Cole Palmer

Chelsea walifungua ukurasa wa mabao dakika ya 22 baada ya beki wa PSG Nuno Mendes kupoteza mpira kwa Malo Gusto.

Ingawa shuti lake la kwanza lilikataliwa na Mendes, Gusto aliokota mpira tena na kumpa Palmer aliyeachwa peke yake katikati, na hakukosea – akiweka mpira kwenye kona ya kushoto mwa lango.

Palmer aliongeza bao la pili baada ya mapumziko mafupi ya dakika ya 30 kwa jitihaada ya kuvutia.

Joao Pedro

Akiwa amepokea pasi safi kutoka kwa Levi Colwill, alikata ndani kabla ya kudanganya beki kwa kuonyesha kana kwamba anapiga pasi, kisha kufyatua shuti kali lililomshinda kipa na kutinga kona ya chini kushoto.

Baada ya hapo, Palmer aligeuka kuwa mtoa pasi, akichanja mbuga upande wa kulia kabla ya kumpasia Joao Pedro ambaye aliupokea mpira vizuri, akaepuka mtego wa kuotea na kumchipia kipa Gianluigi Donnarumma kwa ustadi mkubwa.

Mateso ya PSG yalihitimishwa dakika ya 83 pale Joao Neves alipotolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumvuta nywele Marc Cucurella kwa hasira.

Robert Sanchez

Tukio hilo liliibua vurugu kubwa uwanjani mara baada ya mechi kumalizika, huku kocha Luis Enrique akionekana kumpiga Joao Pedro usoni, pamoja na kipa Donnarumma kujihusisha katika tafrani hiyo.

FIFA ilianza kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya aina hiyo miaka miwili iliyopita, na PSG walimaliza mechi wakiwa na wachezaji 10.

Nahodha wa Chelsea Reece James anyanyua taji baada ya kipenga cha mwisho

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved