logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fulham v Chelsea MOJA KWA MOJA

Mechi ya London derby inayokuja wakati mgumu kwa Chelsea huku mabadiliko ya kiufundi yakitikisa msimu wao wa Ligi Kuu.

image
na Tony Mballa

Michezo07 January 2026 - 22:28

Muhtasari


  • Mchuano wa Chelsea dhidi ya Fulham ugani Craven Cottage unakuja wakati nyeti kwa The Blues, ambao wanatafuta mwelekeo mpya baada ya kuondoka kwa kocha Enzo Maresca.
  • Chelsea wanashika nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu England wakiwa na pointi 31, lakini pengo la pointi 17 dhidi ya viongozi Arsenal linaakisi changamoto kubwa iliyopo mbele yao katika mbio za ubingwa.

Fulham wamevunja ukimya dakika ya 55 kupitia Raúl Jiménez, aliyepachika mpira wavuni kwa shuti la hakika kufuatia pasi murwa. Goli hilo linawaweka wenyeji mbele ya Chelsea 1–0, huku hali ugani Craven Cottage ikizidi kupamba moto.

22' Marc Cucurella alishwa kadi nyekundu. The Blues wanabaki wachezaji kumi ugani.

1' Muamizi anapuliza kipenga chake kuashiria mwanzo wa mechi... Mchuano wa Chelsea dhidi ya Fulham ugani Craven Cottage unakuja wakati nyeti kwa The Blues, ambao wanatafuta mwelekeo mpya baada ya kuondoka kwa kocha Enzo Maresca.

Chelsea wanashika nafasi ya tano kwenye jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza wakiwa wamezoa jumla ya alama 31, lakini pengo la pointi 17 dhidi ya viongozi Arsenal linaakisi changamoto kubwa iliyopo mbele yao katika mbio za ubingwa. Je, watatamba chini ya Calum McFarlane? Tony Mballa

Makala Zinazohusiana

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved