Huenda mwanariadha wa Kenya Mark Otieno akakosa kuhusishwa kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea jijini Tokyo, Japan baada yake kusimamishwa kwa muda kufuatia matokeo ya maabala yalioyoashiria kuwa alikuwa ametumia dawa za kusisimua misuli.
Otieno alikuwa anatarajiwa kushindana kwenye mbio za mita 100 baadae alasiri ya leo.
Sampuli ya mkojo ambayo mwanariadha huyo alipatiana kwenye maabala mnamo Julai 28 iliashiria kuwa alikuwa ametumia dawa za kusisimua misuli.
Hata hivyo, Timu Kenya imeomba kupimwa tena kwa sampuli nyingine baada ya Otieno kusema kuwa hana hatia.
Timu Kenya inashuku kuwa huenda kulikuwa na mchanganyiko wa sampuli katika maabala ambako vipimo vilifanyika.
Otieno ambaye rekodi yake bora zaidi msimu huu ni sekunde 10.05 alikuwa anatarajiwa kukimbia saa nane kasorobo.