logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Niliona kumuacha Kipchoge inawezekana-Gabriel Geay

Chebet alimshinda Gabriel Geay wa Tanzania hadi nafasi ya pili kwa saa 2:06:04

image
na Radio Jambo

Habari18 April 2023 - 15:33

Muhtasari


  • Mwanariadha mwingine wa Kenya Evans Chebet alimshinda Benson Kipruto na kutetea vyema taji lake la Boston Marathon nchini Marekani.
alimaliza wa sita katika Boston Marathon.

Mwanariadha wa Tanzania Gabriel Geay jana Jumatatu alishinda kwa kumaliza wa pili katika mbio kongwe zaidi Duniani za 127 za Boston nchini Marekani kwa kumaliza mbio za Kilomita 42 kwa 2:06:04.

Hata hivyo Geay aliwashangaza wengi baada ya kumpiku mkongwe na ambaye amekua akishikilia rekodi mbalimbali za Dunia katika riadha Eliud Kipchoge kutoka Kenya tukio ambalo ni nadra kwa mwanariadha wa Tanzania.

Mwanariadha mwingine wa Kenya Evans Chebet alimshinda Benson Kipruto na kutetea vyema taji lake la Boston Marathon nchini Marekani.

Chebet alimshinda Gabriel Geay wa Tanzania hadi nafasi ya pili kwa saa 2:06:04 huku Kipruto akimaliza wa tatu kwa saa 2:06:06.

Lakini mwanariadha kutoka Tanzania Gabriel Geay ambaye anashikilia rekodi ya mbio kwa taifa la Tanzania na kushika nafasi ya pili huko Boston Jana Jumatatu anazungumziaje ushindi huo? Amezungumza na Scolar Kisanga

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved