logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu kwa nini David Raya wa Arsenal tayari ameshinda Golden Glove ya EPL 2023/24

Kipa wa Arsenal David Raya ni mshindi rasmi wa tuzo la Golden Glove kwa msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza wa 2023/34.

image
na Samuel Maina

Michezo04 May 2024 - 06:38

Muhtasari


  • •Kipa wa Arsenal David Raya ni mshindi rasmi wa tuzo la Golden Glove kwa msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza wa 2023/34.
  • •Klabu ya Arsenal imesalia na mechi tatu za kucheza, hivyo Raya bado ana nafasi ya kucheza mechi nyingi bila kufungwa.

Kipa wa Arsenal David Raya ni mshindi rasmi wa tuzo la Golden Glove kwa msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza wa 2023/34.

‘Golden Glove’ ni tuzo ambalo hushindwa na walinda lango ambao wamecheza mechi nyingi bila kufungwa bao.

Huku timu nyingi za EPL zikiwa zimecheza mechi kati ya 34 na 36 kila moja hadi sasa, David Raya tayari amecheza mechi kumi na nne bila kufungwa.

Kipa huyo Mhispania alihakikishiwa kushinda ‘Golden Glove’ kwa msimu huu baada ya mpinzani wake wa karibu Jordan Pickford kushindwa kuweka cleansheet siku ya Ijumaa jioni wakati wa mechi ya Everton dhidi ya Luton Town. Pickford sasa amecheza mechi 12 bila kufungwa.

Matokeo ya Ijumaa yanamaanisha kuwa hakuna kipa anayeweza kuweka cleansheet zaidi ya David Raya wa Arsenal msimu huu kwani kila klabu inasalia na mechi 2-4 pekee za kucheza. Hata hivyo, inawezekana kwa Raya na Pickford kugawana tuzo hilo ikiwa kipa huyo wa Everton atafanikiwa kucheza mechi mbili zilizosalia bila kufungwa, naye Raya afungwe katika mechi zote tatu za Arsenal zilizosalia.

Klabu ya Arsenal imesalia na mechi tatu za kucheza, hivyo Raya bado ana nafasi ya kucheza mechi nyingi bila kufungwa.

Mara ya mwisho kwa kipa wa Arsenal kushinda glovu ya dhahabu ilikuwa ni msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza 2015/16 wakati Peter Cech alipotunukiwa tuzo hilo baada ya kutofunga mabao katika mechi 16.

Raya yuko kwa mkopo katika Arsenal kutoka Brentford kwa msimu wa EPL 2023/24. Wanabunduki hata hivyo tayari wameonyesha nia ya kumnunua kipa huyo wa Uhispania kikamilifu mwishoni mwa msimu huu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved