Hatua ya Meneja wa Manchester City Pep Guardiola kuongeza kandarasi yake ni "habari njema" kwa Ligi ya Primia, anasema mkufunzi wa Liverpool Arne Slot.
Guardiola, ambaye ameiongoza City tangu 2016, amesaini mkataba mpya wa miaka miwili utakaodumu hadi 2027.
City wameshinda mataji sita ya Ligi ya Primia chini ya Guardiola - mara mbili wakizishinda timu za Liverpool zinazonolewa na Jurgen Klopp kwa pointi moja pekee.
The Reds walimaliza mbele ya City na kushinda taji hilo mnamo 2020, na vilabu hivyo viwili vimeanzisha moja ya wapinzani wakuu katika ligi kuu.
Slot alimrithi Klopp msimu wa majira ya kiangazi na ameiongoza Liverpool kileleni mwa Ligi ya Primia pointi tano zaidi ya City iliyo katika nafasi ya pili baada ya michezo 11.
Alipoulizwa kuhusu mkataba mpya wa Guardiola, Slot alisema: "Ni habari njema kwa City na kwa ligi kwa sababu kila mtu anataka mameneja bora na wachezaji bora zaidi hapa.
"Hakika ni mmoja wa wasimamizi bora, labda meneja bora wa ligi.
"Ameshinda mataji manne mfululizo kwa hivyo ni sawa kusema labda ndiye meneja bora wa ligi.
"Kwa upande mwingine, wana wachezaji wengi wa hali ya juu kiasi kwamba, kama angefanya chaguo la kuondoka, nisingetarajia wangeishia mkiani mwa ligi msimu ujao."
Akizungumza akizungumza kabla ya safari ya timu yake kucheza na Southampton siku ya Jumapili, Slot alisema Guardiola ni "mmoja wa mameneja bora zaidi kuwahi kuwa nao"