
Mkufunzi
wa Manchester United Ruben Amorim amependekeza afadhali ampe nafasi kwenye
benchi kocha wake wa makipa Jorge Vital mwenye umri wa miaka 63 badala ya
Marcus Rashford kwa sababu ya ukosefu wa juhudi.
Fowadi
huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27 hajahusika katika kikosi cha United
kwa wiki sita na aliachwa kwa mara nyingine kwa mechi ya ushindi wa 1-0
Jumapili dhidi ya Fulham kwenye Ligi ya Premia.
Amorim amemuweka kando Rashford, baada ya kukasirishwa na maombi yake ya kuondoka na wazo lilikuwa kumhamisha wakati wa dirisha la Januari. Hilo bado haijafanyika ilhali muda unazidi kuyoyoma huku kufungwa kwa dirisha la uhamisho la Januari kukikaribia.
Wakati alipoulizwa kwa nini Rashford hakuwepo kwa mechi ya Jumapili katika uwanja wa Craven Cottage, kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 alimkejeli fowadi huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa kutoonyesha juhudi za mtu kutia bidii ya kiwango cha juu kila siku.
"Siku zote ni sababu sawa - mafunzo, jinsi ninavyoona mwanasoka anapaswa kufanya maishani. Ni kila siku, kila undani, "alisema Amorim.
Mreno huyo aliendelea kuweka wazi kuwa hayuko tayari kuwapa nafasi wachezaji ambao hawafanyi vizuri kila siku.
"Kama mambo hayatabadilika, sitabadilika, ni hali sawa kwa kila mchezaji, ukifanya mambo ya juu na sahihi tunaweza kumtumia kila mchezaji. Unaweza kuona kwenye benchi tunakosa kasi kidogo kwenye benchi, lakini ningemweka [kocha wa makipa wa Manchester United Jorge] Vital kabla ya mchezaji ambaye hatoi kiwango cha juu kila siku,” aliongeza.
Awali, vyanzo vya karibu na Rashford vilidai kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hana tatizo na Amorim na alikuwa tayari kuichezea klabu hiyo tena.
Matumaini ya kuhamia AC Milan yamezimwa na ujio wa Kyle Walker kwani klabu hiyo ya Italia inaweza kusajili mchezaji mmoja tu wa Uingereza mwezi huu.
Mkopo unaowezekana kwa Barcelona unategemea kuondoka kwa wachezaji kadhaa na si Eric Garcia au Ansu Fati ambaye ameonyesha nia ya kuondoka Nou Camp.