
Mlinzi wa klabu ya Chelsea Renato Veiga ameondoka na kujiunga na timu ya Juventus ya Italia kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu
Beki huyo wa Chelsea alijiunga na wanablues kutokea Basel katika majira ya joto. Amekuwa akicheza katika nafasi ya kushoto nyuma. Alionekana mara 18 akichezea Chelsea msimu huu na kufunga magoli mawil na kutoa asisiti moja.
Mkufunzi wa Chelsea Enzo Maresca alimwamini mchezaji huyo na amekuwa akimchezesha kwenye baadhi ya mechi, ila inasemekana Veiga alikua akitaka apewe muda mwingi zaidi uwanjani.
Huenda makubaliano hayo ya mkopo yakawa ya manufaa kwa mchezaji na vilevile kwa vilabu vyote viwili
Juventus wamekubali kugharamia mshahara wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno na kulipa ada ya mkopo. mkataba huo hauhusishi ununuzi wa mchezaji huyo.
Beki wa chelsea Renato Veiga atakamilisha msimu huu akiwa kwenye mkopo katika ligii ya Serie A katika klabu ya Juventus. Veiga alijiungana na wanablue mwezi July akitokea FC Basel na amecheza mechi 18 katika.
Veiga pia ana uwezo wa kujeza kama kiungo wa kati atavalia Jezi nambari 12 katika timu ya Juventus.
Baada ya kukamilika kwa mkopo huo , ameandika kwenye mtandao wake wa Instagram; "Nina furaha kuwa kati ya klabu hii kubwa.
Wakati akiwa chelsea alikua akiwa na matamanio ya kuwa miongoni mwa timu ya kwanza, pia aliwahi kusema kwamba nafasi anayofurahia sana kucheza ni fuli beki bali sio beki wa kushoto nafasi ambayo amekua akichezeshwa na Enzo Maresca wakati akiwa Chelsea