logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Arteta azungumzia kumrejesha Raheem Sterling Chelsea ili kuchukua mchezaji mwingine kwa mkopo

Sterling amekuwa na wakati mgumu kuonesha kiwango kizuri akiwa Arsenal baada ya kupewa nafasi nyingi.

image
na Samuel Mainajournalist

Football24 January 2025 - 14:52

Muhtasari


  • Kocha Mikel Arteta ametupilia mbali wazo la kumrudisha fowadi Raheem Sterling kwa Chelsea ili kusajili mchezaji mwingine.
  • ‘Hatufikirii hilo,’ alisema Arteta.

Kocha Mikel Arteta ametupilia mbali wazo la kumrudisha fowadi Raheem Sterling kwa Chelsea ili kusajili mchezaji mwingine wa Premier League kwa mkopo.

Wanabunduki wamepungukiwa katika nafasi ya mashambulio kufuatia majeraha mabaya waliyopata Bukayo Saka na Gabriel Jesus.

Sterling amekuwa na wakati mgumu kuonesha kiwango kizuri akiwa Arsenal baada ya kupewa nafasi nyingi katika wiki za hivi majuzi na kufanya vibaya. Alitolewa tena katika kipindi cha pili baada ya kuanzishwa katika mechi ya Jumatano dhidi ya Dinamo Zagreb.

Huku kipa Neto pia akiwa kwa mkopo kutoka Bournemouth, Arsenal haitaweza kuajiri mchezaji mwingine wa Premier League kama suluhu la muda la masuala yao ya ushambuliaji isipokuwa Mbrazil huyo, au Sterling, arejeshwe kwa vilabu vyao kabla ya muda uliopangwa.

‘Hatufikirii hilo,’ alisema Arteta ghafla alipoulizwa kama mojawapo ya mikataba ya sasa ya mkopo ya Arsenal inaweza kukatizwa.

Huku ikitarajiwa kuwa Bukayo Saka atarejea kabla ya mwisho wa msimu huu, kampeni ya Gabriel Jesus 2024/25 imekamilika baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti mapema wiki hii.

Huku Ethan Nwaneri akiwa amekosa michano minne kabla ya kurejea katikati ya wiki, Arteta amekuwa akiwategemea sana Leandro Trossard na Gabriel Martinelli katika maeneo mengi. Hii imeonyesha hitaji la wazi la mshambuliaji wa Arsenal haraka iwezekanavyo.

Wanabunduki wamehusishwa na wachezaji kadhaa mwezi huu lakini wachezaji kama Benjamin Sesko na Alexander Isak wanaonekana kutokuwa na uwezekano wa kuhama Januari.

Matheus Cunha, wakati huohuo, amekuwa na ofa nyingi na haijulikani anapendelea nini huku Chelsea, Spurs na Nottingham Forest pia zikiwania saini yake.

Arteta anasisitiza kuwa anataka kuimarisha chaguo zake huko Arsenal wakiwa bado wanapigania taji la Ligi Kuu ya England na anatazamia kutinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa bila hitaji la mechi ya mtoano.

Kocha huyo wa Arsenal tayari amekubali kuwa klabu yake inafanya kazi kutafuta mchezaji mpya na kuweka wazi kuwa msajili mpya lazima akidhi vigezo fulani.

"Una rasilimali fulani, uwezo wa kuajiri wachezaji fulani, kukuza wachezaji fulani, kutumia wachezaji fulani kutoka akademi. Ni usawa wa kile tunachoweza kufanya," Arteta alisema.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved