
Timu ya Arsenal inayocheza ligii kuu ya Uingereza ilisalimu amri na kuondoka kwenye kombe la Carabao baada ya kukubali kipigo nyumbani na ugenini dhidi ya Newcastle United.
Newcastle imefikia fainali ya kombe la Carabao kwa mara ya pili katika misimu mitatu baada ya ushindi wa 2-0 wa nusu fainali ya pili dhidi ya Arsenal hapo kujumuisha ushindi wa jumla wa mabao 4-0, ugenini na nyumbani.
Jacob Murphy na Anthony Gordon waliwashambulia wanaume wa Mikel Arteta na kuongeza faida waliyoipata katika mechi ya kwanza katika uwanja wa Emirates Januari 7 na kujiwekea nafasi katika uwanja wa Wembley Machi 16.
Newscastle sasa watakabiliana na Tottenham au Liverpool, ambao watacheza katika mechi nyingine ya nusu fainali ya pili leo Alhamisi usiku.
Mara ya mwisho Arsenal kushinda kombe hili ilikuwa katika msimu wa 1992/93 walipoifunga Sheffield Wednesday katika fainali ya 2-1.
Arsenal wameshinda Kombe la Ligi hii mara mbili katika historia yao.
Kampeni ya msimu jana 2023/2024 ulikuwa wa masikitiko kwa Gunners ambao walifanikiwa kufika raundi ya 16 dhidi ya West Ham.
Walipoteza 3-1 katika uwanja wa Emirates katika mchezo ambao Ben White alijifunga bao la kwanza. Hammers kisha wakafunga tena mara mbili na kuifanya 3-0 baada ya dakika 60 kupitia Mohammed Kudus na Jarrod Bowen. Dakika ya 96 nahodha wa klabu hiyo Martin Odegaard akazawazisha bao la kuvuta machozi.
Katika msimu wa 22/23 walipoteza katika raundi 32 dhidi ya Briton.
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta akizungumza kuhusu kupoteza mchuano wao dhidi ya mawahasimu wao Newcastle alisema,
"Tumecheza mechi nyingi sana, kila baada ya siku tatu, na tulijua kuwa huu utakuwa mchezo wa kiwango cha juu. Kihisia ulikuwa mchezo tofauti kuamini tunaweza fikishwa hapo
Tunahitaji kumeza hili - ni ngumu. Tulikuwa na matarajio mengi. Hakuna kitu tunaweza kufanya sasa - tulipaswa kufanya hivyo kwenye uwanjani. Sasa tunahitaji kuangalia mbele.
Makosa ni sehemu ya mpira wa miguu lakini kwa kawaida huwa tunaendana na kutungwa lakini leo tumewapa matumaini. Tuliwaruhusu kukimbia na tulikuwa katika mazingira magumu - ni timu hatari wakati wangeweza kufanya hivyo"