
Manchester City wanaongoza mbio za kumsajili kiungo mshambuliaji wa England na Nottingham Forest mwenye umri wa miaka 25, Morgan Gibbs-White. (Times)..
Manchester United kwa sasa wanaongoza katika mbio zingine za kumsajili mshambuliaji wa Ghana na Bournemouth mwenye umri wa miaka 25, Antoine Semenyo, lakini wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ikiwa ni pamoja na Liverpool na Tottenham Hotspur. (Sky Sports)
Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Sporting, Viktor Gyokeres, mwenye umri wa miaka 26, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden anapendelea kuhamia kwa mahasimu wao Arsenal (A Bola)
Liverpool wanafuatilia kwa karibu hali ya mshambuliaji wa England mwenye umri wa miaka 29, Ollie Watkins, anayechezea Aston Villa wakati huu wakipanga usajili mbadala wa mshambuliaji wa Newcastle na Sweden, Alexander Isak, mwenye umri wa miaka 25, ambaye kuna ugumu kumpata. (Football Insider)
Juventus, Inter Milan na Napoli zote zinataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Norway, Rasmus Hojlund, mwenye umri wa miaka 22, msimu huu wa joto. (Caughtoffside)
Manchester United wataongeza juhudi zao za kumsajili kiungo wa England wa Southampton mwenye umri wa miaka 19, Tyler Dibling, iwapo watafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa kwa kushinda Ligi ya Europa msimu huu. (ESPN)
Fulham wanaendelea kuwa na nia ya kumsajili winga wa Nigeria wa AC Milan, Samuel Chukwueze, msimu huu wa joto baada ya kushindwa kumsajili mwezi Januari mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Calciomercato)
Chelsea na Newcastle wameulizia upatikanaji wa beki wa kati wa Korea Kusini wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 28, Kim Min-jae. (Footmercato)
Everton wamemuweka mshambuliaji wa Denmark wa Monaco mwenye umri wa miaka 22, Mika Biereth, kwenye orodha yao ya wachezaji inaowafuatilia kwa usajili wa majira ya joto. (Teamtalk)
Kiungo wa Newcastle, Lewis Miley, mwenye umri wa miaka 18, anavivutia vilabu kadhaa vya Ligi Kuu England na ile ya Ujerumani, Bundesliga. (Fabrizio Romano), external
Kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp, hana nia ya nafasi yoyote ya ukocha msimu ujao, huku raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 57 akiwa tayari kukataa ofa zozote zitakazotoka Real Madrid au Brazil. (Sky Germany)
Scott Munn anatarajiwa kuondoka Tottenham baada ya miaka miwili kama afisa mkuu wa soka wa klabu hiyo, huku raia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 51 akilaumiwa kwa sehemu kwa matatizo ya majeraha ya klabu hiyo msimu huu. (Mail)