UHAMISHO EPL

Aston Villa yatangaza usajili wa Emiliano Buendia kutoka Norwich

Klabu ya Arsenal ilikuwa inamumezea mate kiungo huyo kwa muda ila zabuni ya Aston Villa ikakubalika kwani ilipiku ile ya Arsenal.

Muhtasari

•Klabu ya Norwich imetangaza kuwa uhamisho wa Buendia ndio mkubwa zaidi kuwahi fanyika katika klabu hiyo.

•Habari zingine kuhusiana na uhamisho huo zitatolewa baada ya vipimo vya kidaktari kukamilika.

Emiliano Buendia baada ya kushinda kombe la Championship na klabu ya Norwich
Emiliano Buendia baada ya kushinda kombe la Championship na klabu ya Norwich
Image: Hisani

Klabu ya Aston Villa imetangaza usajili wa kiungo matata Emiliano Buendia kutoka klabu ya Norwich City.

Kupitia mtandao wa Twitter, klabu hiyo ambayo ilimaliza katika nafasi ya 11 kwenye ligi kuu Uingereza imesema kuwa imefikia makubaliano na klabu ya Norwich kumchukua kiungo huyo.

Huku Emiliano akiwa nchini Argentina kwenye matayarisho ya mchuano wa kuhitimu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya nchi ya Kolombia siku ya Jumanne, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya kidaktari baada ya mechi hiyo” Klabu ya Aston Villa ilitangaza.

Klabu ya Arsenal ilikuwa inamuwinda kiungo huyo kwa muda  pia  ila zabuni ya Aston Villa ikapiku ile ya Arsenal na kwa hivyo kukubalika.

Klabu ya Norwich imetangaza kuwa uhamisho wa Buendia ndio mkubwa zaidi kuwahi fanyika katika klabu hiyo.

Kulingana na ripoti mbali mbali za kitaifa, iligharimu klabu ya Aston Villa takriban poundi milioni 34 na maongezi  mengine juu yake kumfanya Buendia kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi uzwa na klabu ya Norwich.

Habari zingine kuhusiana na uhamisho huo zitatolewa baada ya vipimo vya kidaktari kukamilika.