NOTI FLOW ASEMA ALIDHULUMIWA

Noti Flow azungumzia kilichomfanya achukie wanaume na kuanza kuchumbia mwanamke

Ameeleza kuwa kwa miaka mingi ambayo amekuwa akichumbiana na wanaume amekuja kugundua kuwa wanaume hawajui kupenda kikweli na wanafikiria ngono ni kila kitu.

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo ambaye pia hucheza kwenye kipindi cha Nairobi Diaries kwenye stesheni ya runinga ya K24 amechapisha picha akionyesha majeraha mwilini kutokana kudhulumiwa na mwanaume aliyekuwa anachumbiana naye.

Noti Flow na mpenzi wake Alami
Noti Flow na mpenzi wake Alami
Image: Hisani

Mwanamuziki  na mwigizaji Florence Kutoto almaarufu kama Noti Flow amefunguka kuhusu kilichomfanya kuchukia wanaume na kuanza kuchumbiana na mwanamke.

Kupitia mtandao wa Instagram, Rapa huyo wa miaka 27 ameeleza masaibu ambayo yamemkumba kwenye mahusiano ambayo amekuwa nayo na wanaume hapo awali.

Kile wanaume wamenifanyia ni kuniumiza,kunisikitisha, kunivunja moyo na kunichezea. Mwanaume niliyekuwa na mahusiano naye hivi karibuni alikuwa karibu kuniua!” Noti aliandika huku akiagiza mashabiki kukoma kuzungumzia mambo wasiyojua.

Noti Flow ameeleza kuwa alipata mapenzi ya kweli kwa mwanamke baada ya kupitia mateso mengi kwenye mahusiano na wanaume.

Mwanamuziki huyo ambaye pia hucheza kwenye kipindi cha Nairobi Diaries kwenye stesheni ya runinga ya K24 amechapisha picha akionyesha majeraha mwilini kutokana kudhulumiwa na mwanaume aliyekuwa anachumbiana naye.

Hata hivyo ameeleza kuwa alimshtaki mwanaume huyo na akakamatwa na maafisa wa polisi.

"Gerezani ndimo nyumbani mwa wahalifu kama wale. Usikubali kutupilia mbali maisha yako. Tuko na kesi inaendele mahakamani na nitahakikisha haki inatendeka" Alisema Noti.

Nadhani si hatma yangu kuwa na uhusiano na mwanaume kwa sababu nimejaribu kabisa na nimejitolea kabisa  ila sijapata chochote kizuri kwenye mahusiano hayo. Nimeishi kuamini kuwa kuna mapenzi  na naamini kuwa ikiwa unampenda mtu basi utafanya lolote kwa minajili yao na kuwapa kipaumbele. Utawajulia hali mara kwa mara kujua kana kwamba wako sawa na hutawaumiza” alieleza Noti Flow.

Ameeleza kuwa ndani ya kipindi cha miaka mingi cha miaka mingi ambacho amekuwa akichumbiana na wanaume amekuja kugundua kuwa wanaume hawajui kupenda kikweli  na wanafikiria ngono ni kila kitu.

Ujumbe wa Noti Flow
Ujumbe wa Noti Flow

Wanataka kuwa na wapenzi wengi lakini ni mwiko kwa mwanamke kutokuwa mwaminifu” aliendelea kusema.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa amepata yote aliyotaka kwa mchumba kwa mpenzi wake wa sasa Armaan Alami. Ameeleza kuwa Alami alimsaidia sana kushinda trauma ya uhusiano wake wa hapo awali, akamfanya mzima tena na kufanya moyo wake kutabasamu tena.

Nilipata mapenzi ya kweli. Ndio, kwa mwanamke. Yeye ni kila kitu nilitaka kwa mchumba. Ananipenda kikweli na hana nia ya kuniumiza. Ningekataa tama na mapenzi ila alinipa matumaini. Sina shaka kuwa yeye ni mpenda roho wangu” Noti Flow alimalizia kwa kusema.