Ramos atia saini mkataba wa miaka miwili na PSG

. PSG itakuwa timu yake ya tatu kuwakilisha

Muhtasari

•Ramos ambaye mkataba wake na Real ulitamatika mwishoni mwa msimu wa 2020/21 ametia saini ya miaka miwili na mabingwa mara tisa wa kombe la ligue 1 nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain.

Sergio Ramos
Sergio Ramos
Image: PSG

Baada ya kuichezea klabu ya Real Madrid kwa kipindi cha miaka 16, hatimaye mlinzi Sergio Ramos ataiwakilisha klabu nyingine msimu ujao.

Ramos ambaye mkataba wake na Real ulitamatika mwishoni mwa msimu wa 2020/21 ametia saini ya miaka miwili na mabingwa mara tisa wa kombe la ligue 1 nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain.

Raia huyo wa Uhispania alicheza katika mechi 671 na Real Madrid na kufunga mabao 101. Ametajwa kama mmoja wa walinzi bora duniani huku akitajwa katika nafasi ya saba kwenye orodha ya tuzo la Ballon d'Or mwaka wa 2017.

Ramos ambaye ana umri wa miaka 35 alianza taaluma yake ya kucheza kandanda  mwaka wa 2003 na klabu ya Sevilla. PSG itakuwa timu yake ya tatu kuwakilisha.