Lionel Messi akubali punguzo la mshahara wake ili kusalia Barcelona hadi 2026

Makubaliano hayo yanashirikisha kupunguza mapato yake hadi nusu ya mshahara wake.

Muhtasari

•Messi, 34, alikuwa mchezaji huru baada ya kandarasi yake ambayo ilikuwa ikimlipa £123m kwa msimu kukamilika tarehe 30 mwezi Juni .

•Messi ndiye mfungaji bora kuwahi kuonekana Barcelona akiwa na magoli 672 na kushinda mataji 10 ya La Liga, mataji manne ya klabu bingwa Ulaya mataji saba ya Copa del rey pamoja na kuwania taji la Ballon d'Or kwa mara ya sita

Image: TWITTER//BBC

Lionel Messi amekubali kusalia Barcelona katika kandarasi ambayo itamuweka katika klabu hiyo hadi 2026 .

Makubaliano hayo yanashirikisha kupunguza mapato yake hadi nusu ya mshahara wake.

Tangazo hilo linategemea kuondoka kwa wachezaji ambapo litaiwezesha Barca kufadhili mshahara wa nahodha huyo wa Argentina.

Messi, 34, alikuwa mchezaji huru baada ya kandarasi yake ambayo ilikuwa ikimlipa £123m kwa msimu kukamilika tarehe 30 mwezi Juni .

Kwa sasa mchezaji huyo yupo likizo baada ya kushinda kombe la Copa America na maelezo ya ndani kuhusu kandarasi hiyo hayajakamilishwa.

Kumshawishi Messi kusalia katika klabu hiyo ndio lililokuwa lengo la mwenyekiti mpya wa klabu hiyo Joan Laporta.

Barca pia inatazamia makubaliano ya kubadilishana wachezaji yanayohusisha uhamisho wa mshambuliaji Antoine Griezmann na kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez , ili kupunguza matumizi ya mishahara ya wachezaji.

Wchezaji kama vile Junior Firpo, Jean Clair Todipo na Carles Alena tayari wameuzwa ili kupunguza matumizi lakini pia uuzaji wa wachezaji wenye majina makubwa pia utafanyika.

Messi alihusishwa na uhamisho wa kuelekea PSG na Manchester City , ambapo angekutana tena na mkufunzi wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola , pamoja na ligi ya MLS nchini Marekani ambapo alisema kwamba huenda akaichezea katika siku za usoni.

Messi ndiye mfungaji bora kuwahi kuonekana Barcelona akiwa na magoli 672 na kushinda mataji 10 ya La Liga, mataji manne ya klabu bingwa Ulaya mataji saba ya Copa del rey pamoja na kuwania taji la Ballon d'Or kwa mara ya sita.