Mwanasoka wa Ufaransa, Jean-Pierre Adams, ambaye alikuwa amekosa fahamu kwa miaka 39 aaga dunia

Kifo cha Adams kimethibitishwa na magazeti ya Ufaransa.

Muhtasari

•Mzaliwa huyo wa Dakar, Senegal alipoteza fahamu akiwa na umri wa miaka 34 kufuatia kosa la 'anaesthesia' alipokuwa anapasuliwa goti kufuatia jeraha mnamo Machi 17, 1982.

Image: AFP

Mwanasoka wa kitambo wa timu ya kitaifa ya Ufaransa  Jean-Pierre Adams, ambaye amekuwa kwenye  'coma' tangu mwaka wa 1982 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 73.

Kifo cha Adams kilithibitishwa asubuhi ya Jumatatu  katika hospitali ya chuo kikuu cha Nimes baada yake kukosa fahamu kwa kipindi cha miaka 39.

Mzaliwa huyo wa Dakar, Senegal alipoteza fahamu akiwa na umri wa miaka 34 kufuatia kosa la 'anaesthesia' alipokuwa anapasuliwa goti kufuatia jeraha mnamo Machi 17, 1982.

Kabla ya upasuaji uliomletea madhara yale kufanyiwa, mlinzi huyo ambaye alichezea Ufaransa kwenye mechi 22 aliripotiwa kuwa mzima na tayari kufanyiwa upasuaji.

Image: GETTY IMAGES

Adams alipewa madawa ya kumfanya apoteze fahamu kwa kipindi cha masaa machache ili afanyiwe upasuaji bila kuhisi uchungu ila  hakuwahi amka baada ya upasuaji huo.

Kifo cha Adams kimethibitishwa na magazeti ya Ufaransa.