Timu ya taifa ya soka Harambee Stars haijapata ushindi wowote kwenye mechi tatu za kufuzu kwa kombe la dunia ambazo zimechezwa hivi karibuni.
Mechi iliyochezwa usiku wa Alhamisi kati ya Harambee Stars na Mali imeibua ghadhabu kubwa mitandaoni miongoni mwa mashabiki wa soka nchini ambao wameeleza kutoridhika kwao.
Harambee Stars walipoteza 5-0 dhidi ya wenyeji wao kwenye mechi yake ya tatu katika kundi E, matokeo ambayo yameacha wengi wakimnyooshea rais wa Shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa kidole cha lawama.
Our Kenyan football problems, in a single photo. Don't go any further. Nick Mwendwa. Corrupt. Compromised. A conduit for cartels. Unfit to govern. pic.twitter.com/kgHLGpMENE
— Lord Abraham Mutai (@ItsMutai) October 7, 2021
Nick mwendwa came and messed up the Kenyan football..We will never qualify for World Cup until, we remove this man in our Soccer. He is fully corrupt, he can’t take any advice, the man is completely senile. The lame came coach was just promoted to a better team #HarambeeStars pic.twitter.com/kTzkMoGrSe
— Arthur Guinness (@Arthurguinness5) October 7, 2021
Uteuzi wa kocha Engin Firat mwezi uliopita uliizua gumzo kubwa mitandaoni wengi wakionekana kukosoa hatua hiyo.
Nick Mwendwa appointed Engin Firat to coach Harambee Stars on a two-month contract. Firat was previously coach of Moldova, where he won 0 matches. Moldova is 75 places below Kenya in FIFA rankings.
— FERDINAND OMONDI (@FerdyOmondi) October 7, 2021
We need to start asking whether Nick is just laundering money with FKF.
Baadhi ya wakenya walihoji jinsi Mwendwa alivyoafikia uteuzi huo huku wakieleza wasiwasi wao kuhusiana na matokeo hafifu ambayo kocha Firat ameandikisha na timu ambazo amekuwa akisimamia hapo awali.
Takriban wiki tatu baadae wasiwasi kuhusiana na uamuzi huo umeongezeka baada ya ndoto za Harambee Stars za kushiriki katika kombe la dunia mwaka ujao kuangamizwa zaidi na Mali.
This man came from Moldova,FIFA ranking at position 180..@Harambee__Stars FIFA ranking is at position 102, it’s like a CBC Pupil teaching a university graduate about the future! Tutapigwa mpaka tuseme nani aliua Lucky Dube 😂😂😂#HarambeeStars pic.twitter.com/OF7866C1J1
— Arthur Guinness (@Arthurguinness5) October 7, 2021
Baadhi ya wanamitandao wamehusisha rais wa FKF Nick Mwendwa na masaibu ambayo yamekumba Harambee Stars.
Kiongozi huyo aliangaziwa sana kwenye mtandao wa Twitter asubuhi ya Ijumaa huku baadhi ya wanamitandao wakimshinikiza ajiuzulu.
Bwana things are thick we've even substituted our goalkeeper for the second half. The only thing remaining is to substitute Nick Mwendwa with a better motivational speaker.
— Gabriel Oguda (@gabrieloguda) October 7, 2021
Je, maoni yako ni yepi kuhusu masaibu ya Harambee Stars?