logo

NOW ON AIR

Listen in Live

FIFA: Kenya yaporomoka hadi 103

Kenya yaporomoka kutoka 102 hadi 103 katika msimamo wa FIFA

image
na Davis Ojiambo

Michezo10 February 2022 - 12:41

Muhtasari


  • • Timu ya taifa Harambee Stars imeporomoka nafasi moja kutoka 102, hadi 103 katika msimamo wa FIFA uliotolewa mapema Februari 10.
  • • Barani Afrika, mabingwa wapya wa kombe la AFCON, Senegal wanazidi kudedea kileleni
  • • Belgium bado inazidi kushikilia nafasi ya kwanza kote duniani huku

Timu ya taifa Harambee Stars imeporomoka nafasi moja kutoka 102, hadi 103 katika msimamo wa FIFA uliotolewa mapema Februari 10.

Harambee Stars imeporomoka baada ya kushindwa kufuzu michuano ya AFCON iliyokamilika wikendi iliyopita nchini Cameroon.

Barani Afrika, mabingwa wapya wa kombe la AFCON, Senegal wanazidi kudedea kileleni wakifuatiwa na Morocco, Nigeria, Misri na Tunisia wakifunga orodha ya timu za taifa tano bora barani Afrika kwa usanjari huo.

Katika msimamo huo wa FIFA, timu ya taifa ya Belgium bado inazidi kushikilia nafasi ya kwanza kote duniani huku ikifuatiwa na Brazil, Ufaransa, Argentina na Uingereza ikiwa imefunga tano bora kote duniani.

Katika ukanda wa Afrika mashariki, timu ya taifa ya Uganda inazidi kuongoza kwa kushikilia nafasi ya 84 kote duniani ikifuatiwa na timu ya Kenya (103), Tanzania (132), Rwanda (136), Burundi (141) huku Sudan Kusini ikiwa ya mwisho kwenye ukanda huu kwa kushikilia nafasi ya 168.

Kwa upande wa soka ya kina dada, Harambee Starlets inashikilia nafasi ya 145

Kuporomoka huku kwa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars kulitarajiwa na wadadisi wengi wa soka nchini kwani kumekuwa na misukosuko katika uongozi wa soka nchini huku FKF ikimuachisha kazi aliyekuwa rais wa shirikisho hiloNick Mwendwa na Waziri wa Michezo Balozi Amina Mohammed akateua kamati ya mpito ili kuongoza shirikisho baada ya visa vya ufisadi kukumba uongozi wa awali wa shirikisho hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved