logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwisho wa reli kwa Ronaldo na Man-U, Picha yake kubwa yaondolewa Old Trafford

Video za picha hiyo kubwa ikiondolewa Old Trafford zimezua mgawanyiko mkubwa miongoni mwa mashabiki.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku17 November 2022 - 06:01

Muhtasari


• Baadhi ya taarifa zilihoji kuwa picha hiyo ilibidi kuondolewa kwa sababu Old Trafford utatumiwa kuandaa fainali za raga ya kina dada na wanaume.

United yaondoa picha za Ronaldo Old Trafford

Ukisema ni mwisho wa reli katika safari yamchezaji Christiano Ronaldo ndani ya timu ya Mnachester United, hutakuwa unakosea.

Hii ni baada ya video kusambazwa mitandaoni ikionesha timu ya Manchester United wakiondoa picha kubwa ya Cristiano Ronaldo mbele ya Old Trafford ili iweze kubadilishwa na jina la Kombe la Dunia la Rugby League kabla ya wikendi hii.

“Cranes wamekuwa kwenye uwanja wa United siku ya Jumatano kusaidia katika kuondolewa kwa bango la Ronaldo kwenye ukumbi wa Old Trafford, siku ambayo sehemu ya kwanza ya mahojiano yake na Piers Morgan yanatarajiwa kutangazwa,” jarida la Manchester Evening News liliripoti.

Lakini inafahamika kwamba bango hilo lilipaswa kuondolewa wiki hii, huku uwanja huo ukiwa mwenyeji wa fainali ya Kombe la Dunia la Ligi ya Raga ya wanaume na wanawake Jumamosi.

Picha za bango la Ronaldo likiwa linabomolewa zimevutia hisia baada ya kubainika kuwa alifanya mahojiano ya moto na Piers Morgan, ambayo yataonyeshwa kwa ukamilifu Jumatano na Alhamisi usiku kwenye TalkTV.

Sehemu za kwanza za mahojiano hayo zilitolewa kwenye mitandao ya kijamii Jumapili usiku na zilionyesha Ronaldo akiituhumu klabu hiyo kwa "kumsaliti" na fowadi huyo akisema hamheshimu Erik ten Hag.

Mahojiano hayo yalimwagwa saa chache baada ya United kuifunga Fulham 2-1 katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu kabla ya msimu kuchukua mapumziko kwa Kombe la Dunia. Ronaldo sasa yuko Qatar na wachezaji wenzake wa Ureno kabla ya mchuano unaoanza Jumapili.

United ilitoa taarifa siku ya Jumatatu baada ya klipu za kwanza kuonekana kwenye mahojiano hayo. Ilisomeka hivi: “Manchester United inabainisha taarifa za vyombo vya habari kuhusu mahojiano na Cristiano Ronaldo. Klabu itazingatia majibu yake baada ya ukweli kamili kujulikana.”

Alipoulizwa kama United walikuwa wanajaribu kumfukuza nje kwa nguvu, Ronaldo alimwambia Piers Morgan Uncensored: "Ndiyo. Sio tu kocha, lakini watu wengine wawili au watatu ndani ya klabu."

Alipoulizwa kama walikuwa katika ngazi ya kocha mkuu, Ronaldo aliendelea: "Ndiyo. Nilihisi kusalitiwa. Kusema kweli, sipaswi kusema hivyo, sijui. Lakini sijali, watu wanapaswa kusikiliza. Najisikia kusalitiwa na mimi niliona kuwa baadhi ya watu hawakunitaka hapa, si mwaka huu tu bali mwaka jana pia."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved