Kombe la Dunia 2022: Mauzo ya bia yapigwa marufuku katika viwanja vya Kombe la Dunia nchini Qatar

Mabadiliko ya msimamo huo yamefanywa siku mbili kabla ya Kombe la Dunia kuanza Jumapili

Muhtasari

• Wale walio katika maeneo ya biashara ya viwanja kwenye mashindano bado wataweza kununua pombe.

Image: BBC

Pombe hazitauzwa katika viwanja vinane vya Kombe la Dunia nchini Qatar, Fifa imetangaza.

Pombe ilipangwa kutolewa "katika maeneo maalum ndani ya viwanja", licha ya uuzaji wake kudhibitiwa vikali katika nchi hiyo ya Kiislamu.

Wale walio katika maeneo ya biashara ya viwanja kwenye mashindano bado wataweza kununua pombe.

Mabadiliko ya msimamo huo yamefanywa siku mbili kabla ya Kombe la Dunia kuanza Jumapili wakati Qatar itakapocheza na Ecuador.

"Baada ya majadiliano kati ya viongozi wa nchi wenyeji na Fifa, uamuzi umefanywa kulenga uuzaji wa vileo kwenye tamasha la mashabiki wa Fifa, maeneo mengine ya mashabiki na kumbi zilizo na leseni, kuondoa sehemu za mauzo ya bia kwenye viunga vya uwanja wa Fifa Kombe la Dunia 2022," ilisema taarifa ya shirikisho la soka duniani.

"Hakuna athari kwa uuzaji wa Bud Zero ambayo itaendelea kupatikana katika viwanja vyote vya Kombe la Dunia la Qatar.

"Mamlaka za nchi mwenyeji na Fifa zitaendelea kuhakikisha kwamba viwanja na maeneo ya jirani yanatoa uzoefu wa kufurahisha na wa heshima kwa mashabiki wote.