Mfukufunzi wa zamani wa Leeds Marcelo Bielsa amechukuwa hatamu za ukufunzi katika timu ya Taifa ya Uruguay.
Mkufunzi huyo alipigwa kalamu baada ya msururu wa matokeo mabaya katika klabu ya Leeds kwenye ligi kuu nchini Uingereza.
Aidha meneja huyo ni moja wapo wa wakufunzi wanaoenziwa sana katika ulingo wa soka duniani na hata meneja wa timu ya Manchester City pep Guardiola amewai msifia akisema kuwa Bielsa ni mojawapo wa wakufunza bora duniani.
Bielsa, anatarajiwa kutia saini kandarasi ya mkataba wake utakao dumu hadi Kombe la Dunia 2026 huku Uruguay ikimwamini kwa mradi wao wa muda mrefu.
"Atajiunga nasi katika siku zijazo, hatimaye yote yamekubaliwa", mjumbe wa Shirikisho la soka nchini Uruguay Jorge Casales alithibitisha.
Mwanahabari tajika wa maswala ya uhamisho wa wanasoka Fabrizio Romano alitangaza haya katika akaunti yake ya Instagram.
Bielsa amewai zifunza timu ya taifa ya Argentina, Chile, timu ya Atletico Bilbao, Marseille, Lille, Lazio na timu ya Leeds.