logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Liverpool yamsajili Kiungo wa Brighton, Mac Allister

Liverpool wamekamilisha usajili wa Alexis Mac Allister kwa kandarasi ya miaka mitano kwa pauni 55.

image
na Davis Ojiambo

Michezo08 June 2023 - 13:47

Muhtasari


  • • Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga mabao 20 katika mechi 112 akiwa na Seagulls na kuisaidia Argentina kushinda Kombe la Dunia la 2022.
  • • Mac Allister alijiunga na Brighton kutoka Argentinos Juniors Januari 2019 na akarejea katika klabu ya Buenos Aires kwa mkopo.
Wachezaji wa Manchester united na Brighton wakimzunguka mwamuzi Peter Bankes

Liverpool wamekamilisha usajili wa kiungo Alexis Mac Allister kutoka Brighton kwa kandarasi ya miaka mitano kwa kima cha pauni pauni milioni 55.

Mchezaji huyo wa Argentina alikuwa mchezaji muhimu wa klabu ya Brighton ilipomaliza katika nafasi ya sita kwenye Ligi ya kuu ya Uingereza msimu uliopita na kufuzu kwa mashindano ya Uropa kwa mara ya kwanza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga mabao 20 katika mechi 112 akiwa na Seagulls na kuisaidia Argentina kushinda Kombe la Dunia la 2022.

"Ninahisi nimejawa na furaha. Ni ndoto iliyotimia na siwezi kusubiri kuanza," alisema Mac Allister.

"Nilitaka kuhusika na maandalizi ya msimu ujao, kwa hivyo ni vizuri kwamba kila kitu kimekamilika. Ninatazamia kukutana na wachezaji wenzangu.

"Ulikuwa mwaka mzuri kwangu - Kombe la Dunia, kile tulichofanikiwa na Brighton - lakini sasa ni wakati wa kufikiria juu ya Liverpool na kujaribu kuwa mchezaji bora na mwanadamu bora kila siku."

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anatazamia kuimarisha safu yake ya kati huku James Milner, Naby Keita na Alex Oxlade-Chamberlain wakiondoka Anfield msimu huu.

Liverpool walijiondoa  kutoka kinyang'anyiro cha kusaka katika shindano la kupata saini ya mchezaji wa Borussia Dortmund na Uingereza, Jude Bellingham, ambaye anaelekea kujiunga na Real Madrid baada ya klabu hizo kukubaliana euro milioni 103 kwa uhamisho wake.

Mac Allister alijiunga na Brighton kutoka Argentinos Juniors Januari 2019 na akarejea katika klabu ya Buenos Aires kwa mkopo.

Mac Allister aliimarisha nafasi yake katika timu ya taifa ya Argentina na amewachezea washindi hawa wa kombe la dunia mara 16 na kuibuka kama mchezaji bora wakati wa ushindi wao wa tatu wa Kombe la Dunia mwezi Desemba.

Baada ya kupoteza mechi yao ya kwanza na Saudi Arabia, kisha alianza michezo sita iliyofuata kwa timu ya Lionel Scaloni.

“Tangu niliposhinda Kombe la Dunia, nilisema kwamba nataka kushinda mataji zaidi na nadhani klabu hii itanisaidia kufanya hivyo,” alisema Mac Allister.

"Hilo ndilo lengo na unapokuwa kwenye klabu kubwa kama hii lazima ushinde mataji. Naona jinsi klabu hii ilivyo kubwa - wachezaji tulionao, wafanyakazi, kila mtu. Nimefurahishwa sana na ninatarajia kuchezea klabu hii."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved