logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu Tetesi za uhamisho bara Uropa

Habari za tetesi za uhamisho wa soka ya bara Uropa zimeenea mitandaoni. Je, wafahamu gumzo katika soko la uhamisho?

image
na TOM KIRIMI

Michezo05 July 2023 - 10:59

Muhtasari


  • • Man City tayari walishapata saini ya kiungo wa Chelsea Mateo Kovacic baada ya kubanduliwa nje katika shindano na Arsenali katika kupata saini ya Declan Rice.
  • • Arsenal walilazimika kutoa pauni 105 ili kuweza Declan Rice huyo katika uga wa Emirates.
Declan Rice, Mason Mount, Josko Gravidiol.

Habari za tetesi za uhamisho wa soka ya bara Uropa zimeenea mitandaoni. Je, wafahamu gumzo katika soko la uhamisho? Usiwe na wasiwasi. Meza ya Radio Jambo inaangazia kukuletea taarifa hii moja kwa moja wakati wa dirisha ya uhamisho wa msimu wa joto.

Mason Mount mwenye umri wa miaka 24, mbaye amekuwa katika timu ya Chelsea kuanzia alipokuwa na umri wa miaka 6 ametamatisha uchunguzi wa hali yake ya kiafya kabla ya uhamisho wake kwa mahasimu wa Chelsea katika ligi ya EPL, Machester United.

Kulingana na Fabrizio Romano, Kiungo wa WestHam, Declan Rice amekaribia kujiunga na timu ya Arsenali.

Vigogo hawa wa EPL wamewapiku wapinzani wao wakuu Manchester City kuipata saini ya mchezaji huyo muhimu wa WestHam.

Arsenal walilazimika kutoa pauni 105 ili kuweza kumleta kiungo huyo katika uga wa Emirates. Arsenali wanaangazia kuongeza nguvu katika kikosi chao baada ya kumsaini Mjerumani Kai Havertz.

Mbali na wachezaji hawa, Timu ya Chelsea imedhibitisha kumsaini mshambulizi kutoka nchi ya Senegal Nicholas Jackson.

Mshambulizi huyo ameondoka VillaReal kwa takribani pauni 35. Chelsea pia imemnyakua winga Diego Moreira kutoka timu ya Benfica. Chelsea pia inaangazia kumpata kiungo wa Brighton Moises Caicedo.

Ikumbukwe kuwa washindi hawa wa klabu bingwa bara Ulaya mwaka wa 2021 tayari walishawasaini Christopher Nkunku kutoka Leipzig na kupata huduma za beki mchanga, Malo Gusto kutoka Lyon ya Ufaransa.

Mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza, Man City wanawinda huduma za beki Josko Gravidiol kutoka Leipzig.

Hata hivyo, Man City tayari walishapata saini ya kiungo wa Chelsea Mateo Kovacic baada ya kubanduliwa nje katika shindano na Arsenali katika kupata saini ya Declan Rice.

Baada ya Real Madrid kumnyakua Jude Bellingham kutoka mababe wa soka Borussia Dortmund kwa pauni milioni 100, sasa waangazia kupata saini ya talanta chipuka Arda Guler kutoka Fenerbahce.

Real Madrid watapoteza meneja wao mwenye tajriba ya hali ya juu Carlo Ancelotti kwa timu ya Brazil msimu ujao.

Kati ya wachezaji tajika wanaoendelea kutoka ligi kuu kutoka bara Ulaya kuelekea ligi ya Saudi Arabia ni Roberto Firmino kuelekea Al Ahli.

Firmino amewaunga mshambulizi wa zamani wa Real Madrid Karim Benzema, Benjamin Mendy kutoka Chelsea, Nahodha wa timu ya taifa ya Senegal Kalidou Koulibally.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved