logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbappe afuatilia asili yake ya Kiafrika katika nchi yake ya babake, Cameroon

Ni ziara ya kwanza kwa Mbappe nchini humo tangu kuwa nyota wa kimataifa.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo07 July 2023 - 11:35

Muhtasari


    aliwasili Cameroon Alhamis

    Mshambulizi matata wa PSG, Kylian Mbappe, yuko nchini Cameroon.

    Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa aliwasili katika jiji kuu nchi hiyo ya Afrika Magharibi, Yaounde siku ya Alhamisi akiwa ameandamana  na baba yake Wilfred Mbappe ambaye alizaliwa katika jiji kubwa la Douala.

    Wawili hao walifika uwanja wa ndege jijini Yaounde na kupokelewa na mashabiki na maafisa wa soka nchini humo.

    Ni ziara ya kwanza kwa Mbappe nchini humo tangu kuwa nyota wa kimataifa.

    Katika ziara hiyo yake ya siku tatu, anatazamiwa kucheza mechi dhidi ya timu ya daraja la pili inayomilikiwa na mchezaji nyota wa zamani wa tenisi, Yannick Noah.

    Mbappe pia atatumia siku chache zijazo kuzuru nchi hiyo, ambapo atakutana na wanahabari pamoja na kushirikisha mamlaka katika msururu wa shughuli.

    Mkameruni huyo mzaliwa wa Ufaransa anatazamiwa kujenga kituo cha burudani na vituo vya kijamii nchini Cameroon.


    RADIO JAMBO FREQUENCIES

    Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


    logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved