logo

NOW ON AIR

Listen in Live

AFCON 2027: CAF yakamilisha ukaguzi wa miundombinu Kenya, Tanzania na Uganda

Mataifa yote matatu yameagizwa kutekeleza kwa pamoja maelekezo yaliyotolewa ili kufikia lengo la Afrika Mashariki kuandaa mashindano hayo.

image
na Radio Jambo

Football03 August 2023 - 03:54

Muhtasari


•Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia amezishukuru Serikali za nchi hizo kwa ushirikiano waliotoa kufanikisha ukaguzi.

•Rais Karia ametoa rai kwa mataifa yote matatu kutekeleza kwa pamoja maelekezo yaliyotolewa ili kufikia lengo la Afrika Mashariki kuandaa mashindano hayo

Timu ya Wakaguzi wa utayari wa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji AFCON 2027, kutoka Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) imehitimisha ukaguzi wao salama Agosti 2, 2023 Zanzibar kwa kikao cha majumuisho kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo wa Tanzania Saidi Yakubu.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia amezishukuru Serikali za nchi hizo kwa ushirikiano waliotoa kufanikisha ukaguzi huo ikiwemo nia ya kuomba kuwa wenyeji wa mashindano hayo.

“Ukaguzi umemalizika vizuri, kwa kweli wameona tupo ‘serious’ na kuna mambo ambayo wametuelekeza tuyafanye, kwa upande wetu kama Tanzania bara na Zanzibar yapo mengi yamefanyika kwa sababu wakandarasi wapo site na vitu vinaonekana, wameelekeza hili jambo hili tulifanye kwa pamoja na wametoa siku 10 ili kukamilisha nyaraka zote zinazohitajika kulingana na maelekezo yao,” amesema Rais Karia.

Aidha, Rais Karia ametoa rai kwa mataifa yote matatu kutekeleza kwa pamoja maelekezo yaliyotolewa ili kufikia lengo la Afrika Mashariki kuandaa mashindano hayo ambayo hayajawahi kufanyika katika ukanda huo na nchi hizo zinatakiwa kukamilisha miundombinu ya michezo itakayotumika kwenye mashindano hayo kabla ya Desemba 2025.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved