Klabu ya Chelsea imetangaza namba za jezi za wachezaji wake 29, wakiwemo wale waliosalia na wale waliosajiliwa mpaka sasa, zikiwa zimesalia siku chache kuelekea kuzinduliwa kwa msimu 2023/24.
Klabu hiyo kupitia tovuti yao rasmi wamechapisha habari hizo zikiambatanishwa na namba ya jezi ambayo kila mchezaji amekabidhiwa.
Wachezaji kadhaa wageni na waliosalia walichagua namba mpya, wachache wakisalia namba walizokuwa nazo misimu ya nyuma.
Kwa haraka, tuliweza kubaini hakuna mchezaji hata mmoja kati ya hao 29 ambaye alikubali kuchukua jezi nambari 9 ambayo kwa muda mrfu imekuwa ikitajwa kama jezi ya mikosi na nuksi.
Jezi namba 9 imekuwa ikihusishwa na mikosi tangu enzi za wachezaji kama Fernando Torres, Romelu Lukaku, Tammy Abraham, Aubameyang miongoni mwa wengine ambao wote viwango vyao wa soka vilishuka baada ya kukabidhiwa jezi hiyo.
Hii hapa ni orodha ya wachezaji wote 29 kila mmoja na namba ya jezi aliyokabidhiwa;
1 - Kepa Arrizabalaga
2 - Axel Disasi
3 - Marc Cucurella
5 - Benoit Badiashile
6 - Thiago Silva
7 - Raheem Sterling
8 - Enzo Fernandez
10 - Mykhailo Mudryk
11 - Noni Madueke
13 - Marcus Bettinelli
14 - Trevoh Chalobah
15 - Nicolas Jackson
16 - Lesley Ugochukwu
17 - Carney Chukwuemeka
18 - Christopher Nkunku
19 - Armando Broja
20 - Andrey Santos
21 - Ben Chilwell
23 - Conor Gallagher
24 - Reece James
26 - Levi Colwill
27 - Malo Gusto
29 - Ian Maatsen
31 - Robert Sanchez
33 - Wesley Fofana
37 - Mason Burstow
47 - Lucas Bergstrom
50 - Eddie Beach
67 - Lewis Hall
Wengi wa wachezaji hao ni makinda walionunuliwa na wengine kupandishwa daraja kutoka timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18.