Barcelona kuondoa kifungua kinywa kwa wachezaji ili kuokoa matumizi ya pesa

Sio siri kwamba Barcelona wamekuwa wakikabiliwa na ugumu wa kifedha kwa miaka michache, na kulazimisha kilabu kufanya maamuzi ambayo hayakupendwa.

Muhtasari

• Katika msimu wa kiangazi wa 2021, ilibidi wamwachie Lionel Messi aondoke katika klabu hiyo kama mchezaji huru baada ya kushindwa kuongeza mkataba wake.

Barcelona wajipata pabaya kwa kumhonga refa
Barcelona wajipata pabaya kwa kumhonga refa
Image: Facebook

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa kutoka Uhispania ni kwamba klabu kubwa Zaidi ya mpira Barcelona imetangaza nia ya kuondoa menyu ya chakula cha asubuhi kwa ajili ya wachezaji wake katika mpango wa kuhakikisha wanaokoa matumizi ya pesa.

Kulingana na jarida la Uhispania Relevo, Barcelona wameamua kuondoa menyu ya kiamsha kinywa kwa wachezaji wachanga ili kuokoa pesa.

Ripoti hiyo inadai kuwa wachezaji hao wa vijana wamekuwa hawatumii fursa ya chakula cha kiamsha kinywa kinachotolewa, jambo ambalo limemfanya rais wa klabu Joan Laporta kuhitimisha kuwa ni gharama zisizostahili.

Sio siri kwamba Barcelona wamekuwa wakikabiliwa na ugumu wa kifedha kwa miaka michache, na kulazimisha kilabu kufanya maamuzi ambayo hayakupendwa na kutoa mwanga kwa mashabiki, Pulse Football walibaini.

Katika msimu wa kiangazi wa 2021, ilibidi wamwachie Lionel Messi aondoke katika klabu hiyo kama mchezaji huru baada ya kushindwa kuongeza mkataba wake. Walijaribu kumrudisha mfungaji bora wao mapema msimu huu wa joto, lakini hawakuweza kupata pesa za kugharamia uhamisho wake wa bure.