Taifa la Uganda limejizolea sifa kote duniani kwa kuwa na wingi wa mashabiki wa kandanda ya ughaibuni haswa ligi kuu ya Premia nchini UIngereza.
Si mara ya kwanza kusikia ripoti kuhusu mashabiki wa timu kubwa nchini humo kama Arsenal, Man United, Chelsea na zingine wakisherehekea ushindi wao hadharani.
Wikendi iliyopita baada ya Arsena kuinyuka United ugani Emitares mabao 3 kwa 1, mashabiki wa Arsenal waliojawa na furaha Jumatatu asubuhi waliandaa tafrija ya kusherehekea ushindi wao katika mitaa wakiwapakulia watoto vyakula.
Wakiwa wamevalia Jezi zao nyekundu za 'Fly Emirates', wafuasi wa Arsenal mjini Jinja wamejitokeza barabarani kusherehekea ushindi wao maarufu Jumatatu.
Waliimba 'Arsenal iliichabanga Man U' na kushikilia bango lililoonyesha matokeo yenye maneno, 'Premier League ni ligi bora zaidi duniani.'
Huku wakiimba na kupiga kelele kwa shangwe, pia walimdhihaki adui yao mkali, wakidai jinsi Man United ni 'ndogo' timu ambayo haiwezi kuifunga Arsenal.
Ikumbukwe mashabiki wa Arsenal wanapenda kufanya maandamano hayo baada ya ushindi dhidi ya adui wao mkubwa.
Itakumbukwa mwezi Januari, kundi la mashabiki wa Arsenal walikamatwa na Polisi kwa kushikilia sawa lakini baadaye waliachiliwa bila kufunguliwa mashtaka.
Upinzani kati ya Arsenal na Manchester United ni moja ya mkali zaidi duniani, na hii ilitengenezwa wakati wa siku za Arsene Wenger na Alex Ferguson.