Mmiliki wa Chelsea anaswa kwenye kamera akikimbizwa na mashabiki wenye hasira

Mashabiki wa Chelsea waliojawa na hasira walimsubiri mmiliki huyo nje ya uwanja wa Stamford Bridge wakitaka malelezo baada ya Chelsea kupigwa nyumbani na Aston Villa Jumapili alasiri.

Muhtasari

• Eghbali, anayekiongoza klabu hiyo pamoja na Todd Boehly, inasemekana aliingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha wachezaji.

Mmiliki wa Chelsea akitoroka mashabiki.
Mmiliki wa Chelsea akitoroka mashabiki.
Image: X

Baada ya kupigwa nyumbani Stamford Bridge na Aston Villa Jumapili alasiri, Mmiliki mwenza wa Chelsea, Behdad Eghbali alionekana akiwakimbia mashabiki waliokuwa na hasira.

Kwa mujibu wa klipu na picha ambazo zimekuwa zikienezwa katika mitandao ya kijamii, Behdad alionekana akikimbia kutoka kwa mashabiki ambao walikuwa wanamfuata kwa kumnyoshea vidole nje ya uwanja wa Stamford Bridge.

Eghbali, anayekiongoza klabu hiyo pamoja na Todd Boehly, inasemekana aliingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha wachezaji ili kukihutubia kikosi baada ya kutocheza vizuri na The Blues, matokeo ambayo yaliwafanya wakazomewe nje ya uwanja na mashabiki wao.

Baada ya mechi hiyo, kipande cha picha ya Eghbali kilisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya mashabiki wa Chelsea wakionekana kumkimbiza na kutaka majibu.

Eghbali alionekana akikimbilia nyuma ya gari jeusi, akisaidiwa na mlinzi.

‘Angalia anakimbia!’ Mfuasi mmoja wa Chelsea alisikika akipiga kelele kwenye kamera kabla ya mlango wa gari kufungwa.

Bahati nzuri ya Chelsea imekuwa ikidorora tangu Boehly na Eghbali wachukue mikoba kutoka kwa Roman Abramovich, na kumaliza vibaya katika nafasi ya 12 msimu uliopita licha ya matumizi makubwa ya klabu kwa wachezaji.

Mambo hayajaboreka msimu huu, huku Washikaji hao wa London Magharibi wakiwa wameshinda mechi moja tu kati ya sita za mwanzo za Ligi Kuu ya Uingereza na shinikizo linaongezeka.